• HABARI MPYA

    Friday, July 13, 2012

    MANJI ATAJA JESHI LAKE LA MIAMVULI, ASEMA AKICHAGULIWA NALO YANGA ITATISHA KINOMA


    Manji akiwa amemuinua mkono Bin Kleb, wengine kulia ni Manyama na Nyambaya, wakati kushoto ni Sanga

    Na Mahmoud Zubeiry
    MGOMBEA Uenyekiti wa klabu ya Yanga, katika uchaguzi wa Jumapili ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam Yussuf Mehboob Manji leo ametambulisha watu watano anaotaka kuchaguliwa nao wakati alipokuwa akihutubia mamia ya wanachama kwenye Mkutano wa kampeni, Uwanja wa Kaunda, uliopo makao makuu ya klabu, makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani.
    Manji aliwataja watu hao kuwa ni nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na Wajumbe wanne ni Abdallah Bin Kleb, Mussa Katabaro, Lameck Nyambaya na George Manyama.
    Ikumbukwe uchaguzi huo mdogo unafuatia Wajumbe wengi wa Kamati ya Utendaji iliyochaguliwa miaka miwili iliyopita, akiwemo Mwenyekiti Wakili Lloyd Baharagu Nchunga na Makamu wake, Davis Mosha kujiuzulu na watakaochaguliwa Jumapili watadumu kwa miaka miwili, kumalizia kipindi cha uongozi cha waliojiuzulu.
    Manji aliwaomba wanachama wa Yanga pamoja na kumchagua yeye Jumapili, pia wawachague na watu hao watano, Sanga, Katabaro, Bin Kleb, Nyambaya na Manyama, kwani ni watu ambao anaamini atafanya nao kazi vizuri na kwa ufanisi.
    Alisema iwapo akichaguliwa watu hao na mambo yakawa mabaya klabuni, atakuwa tayari kujiuzulu lakini akasema atasikitika iwapo atachaguliwa pamoja na watu tofauti nao hao.
    Alisema katika kipindi hiki ambacho klabu haina uongozi, watu hao watano wamekuwa wakimsaidia kujenga timu kama kusajili na kadhalika kwa kujitolea hivyo ana imani nao kwa kiasi kikubwa.
    Shughuli hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa wanachama Vijana wa Yanga, Bakili Mohamed Makele na Mwenyekiti wa Wazee, Mzee Ibrahim Ally Akilimali, ambao waliwaomba wana Yanga kuchagua timu hiyo na mambo yatakuwa mazuri.
    Umati wa wanachama wanaokadiriwa kufika 2000 au zaidi ulihudhuria mkutano huo na wakati wote walikuwa wakishangilia hotuba, kuonyesha kwamba wanaafiki.
    Manji anahutubia

    Manji anahutubia

    Manji anahutubia

    Manji anahutubia kwa hisia kali

    Manji anahutubia kwa msistizo

    Mwenyekiti mtarajiwa Yanga

    Mtu wa kazi, Bin Kleb

    Pentagon inavyoonekana

    Hapa anasema baada ya mwaka mmoja tu wa kuwa madarakani; Yanga itakuwa zaidi ya TP Mazembe

    Manji inabidi ajenge na vyoo uwanjani akichaguliwa; Mzee huyu alishikwa wakati mkutano ukiendelea, akaamua kujisitiri hapa

    Kura za Manji, Sanga, Bin Kleb, Manyama na Nyambaya zikijipoza kwa uji wa mchele

    Watu wanapiga makofi; maana yake jeshi limekubalika 

    Mussa Katabaro anamwaga sera

    Bin Kleb anamwaga sera, alisema yeye si mtu wa maneno, ni mtu wa vitendo

    Nyambaya anamwaga sera

    Kachaa anapiga mzigo wakati mkutano unaendelea

    Sanga kushoto akimsalimu Bin Kleb. Katikati ni Katabaro

    Akina mama nao watampa Manji na timu yake, kura zao

    Manji akipongezana na jembe lake, Bin Kleb

    Hapa aanahidi kulipa kisasi cha 6+5= 11

    Kwa kuingia mkutanoni ilibidi uwe na kadi ya uanachama, basi wasio na kadi waliishia kupiga chabo

    Kampeni zinaendelea kwenye mkutano

    Nyomi

    Ibada zinaendelea sambamba na kusikiliza hotuba za kampeni

    Nyomi

    Rais na Makamu wake wakijadiliana

    Nyomi

    Mzee Akilimali akiwaombea kura vijana kwa hisia zote 

    Rais na Makamu wake wakijipanga mapemaa 

    Manji anamwaga sera

    Hamisi Kiiza 'Diego' akiondoka baada ya kusikiliza kampeni

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANJI ATAJA JESHI LAKE LA MIAMVULI, ASEMA AKICHAGULIWA NALO YANGA ITATISHA KINOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top