| Mussa akipangua msitu wa mabeki |
Hivi sasa Simba SC inatayarisha mkataba kwa ajili ya mshambuliaji
Daniel Akuffo kutoka Hearts Of Oak ya Ghana ambao utapelekwa Arusha, timu hiyo
ilipoweka kambi ausaini.
Habari kutoka Arusha, ambako Simba imeweka kambi kujiandaa
na msimu mpya wa Ligi Kuu, zimesema kwamba katika siku ya kwanza ya mazoezi yao
na kikosi hicho leo, wachezaji wote hao wawili wameonyesha viwango vya hali ya
juu.
Imeelezwa kwamba, mshambuliaji Akuffo ni hatari mno na kwa
haraka haraka hakuna wa kumfananisha naye kati ya washambuliaji wote waliopo
Tanzania kwa sasa.
Anasifiwa kuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki
mpira, kasi, nguvu, ufundi na mbinu za kimchezo- maana yake Wekundu wa Msimbazi
wamelamba dume.


.png)
0 comments:
Post a Comment