• HABARI MPYA

    Tuesday, August 14, 2012

    MATUMLA, MTAMBO WA GONGO TAMTHILIYA KUENDELEA DAR LIVE IDDI MOSI


    Meneja Matukio wa Ukumbi wa Dar Live, Abdallah Mrisho, akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu burudani itakayotolewa siku ya Idd Mosi. Wengine pichani ni Msanii Linah Sanga (wa kwanza kulia), Promota wa ndondi, Kaike Siraj (wa pili kulia), Mratibu wa Burudani Dar Live, Juma Mbizo (wa pili kushoto) na Bondia Maneno Oswald (wa kwanza kushoto).
    Promota wa ndondi, Kaike Siraj akielezea mapambano yatakayokuwepo siku hiyo ya Idd Mosi.
    Maneno Oswald 'Mtambo wa Gongo' akitoa tambo zake jinsi atakavyomchakaza mpinzani wake Rashid Matumla.
    Bondia Rashid Matumla 'Snake Man' nae akijigamba mbele ya wanahabari (hawapo pichani).
    Mabondia hao wakitunishiana misuli.
    Mratibu wa Burudani Dar Live, Juma Mbizo akielezea jinsi walivyojipanga kwa burudani hiyo.Juma Kassim Nature akiahidi burudani ya aina yake siku hiyo.
    Msanii Mwasiti Almasi nae akielezea alivyojipanga kwa ajili ya shoo ya Idd Mosi ndani ya Dar Live.
    Linah Sanga akiwaahidi mashabiki wake kufika kwa wingi Dar Live siku ya Idd Mosi kushuhudia makamuzi ya aina yake
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MATUMLA, MTAMBO WA GONGO TAMTHILIYA KUENDELEA DAR LIVE IDDI MOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top