• HABARI MPYA

    Tuesday, August 14, 2012

    KIFAA CHA CHILE CHATUA MAN UNITED, SASA ASUBIRIWA VAN PERSIE


    MSHAMBULIAJI wa Chile, Angelo Henriquez mwenye umri wa miaka 18, amekamilisha vipimo vya afya katika usajili wake, Manchester United kutoka klabu ya Universidad ya Chile na sasa inasikiliziwa dili ya Robin Van Persie kutoka Arsenal. 
    Kinda huyo aliyeigharimu United pauni Milioni 4, alitumia muda wa saa tatu katika vipimo hospitali ya Bridgewater mjini Manchester jioni hii. Henriquez amefunga mabao 11 katika mechi 17 za ligi mwaka huu, ambao ni wa kwanza akiiwezesha klabu yake, kutwaa taji. 
    United front: Angelo Henriquez (right) is set to seal his move to Old Trafford
    Angelo Henriquez (kulia)
    New recruit: Angelo Henriquez
    Fighting fit: Angelo Henriquez
    Henriquez  baada ya vipimo
     
    Tayari kocha wa United, Sir Alex Ferguson amemsaini Shinji Kagawa na Nick Powell kuelekea msimu ujao na anaendelea kuipigania saini ya Nahodha wa Arsenal, Robin van Persie.
    Kocha wa Gunners, Arsene Wenger hataki kumpoteza mfungaji huyo bora wa Ligi Kuu England, lakini Ferguson anatumai kuinasa saini ya mchezaji huyo kabla ya mechi yao ya ufunguzi ya Ligi Kuudhidi ya Everton Jumatatu. Ilielezea kwamba Ferguson alifanya mazungumzo na ya faragha na Wenger.
    Transfer tussle: Robin van Persie could be heading to Manchester United as soon as this weekend
    Robin van Persie kulia
    Inafahamika kocha wa Arsenal, amerudia msimamo wake kwa kumuambia Ferguson kwamba mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 hataruhusiwa kuhamia United bila dau la pauni Milioni 30 - lakini The Gunners itasikiliza ofa ya kuanzia pauni Milioni 20. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIFAA CHA CHILE CHATUA MAN UNITED, SASA ASUBIRIWA VAN PERSIE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top