Jose Mourinho sasa anataka aitwe 'Only One'
IMourinho akishangilia Scudetto na Inter Milan
Mourinho alishinda Ligi ya Mabingwa na Porto kisha na Inter Milan
KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho anataka kubadilisha jina lake la utani kutoka ‘Special One’ hadi ‘Only One’. "Nipende, usinipende, ni mimi tu niliyeshinda mataji matatu ya ligi kubwa duniani. Hivyo, kwa heshima ya juu ya 'Special One', watu wangeanza kuniita mimi 'Only One',"alisema Mourinho, akihojiwa na kituo cha TV cha SIC cha Ureno. Mourinho anafikiri anastahili jina hilo, baada ya kuibuka kocha wa kwanza kihistoria kushinda mataji katika Ligi Kuu tatu kubwa Ulaya, England, Itali na Hispania. Mreno huyo ameshinda La Liga na Real Madrid msimu uliopita baada ya kushinda Seire A na Inter Milan na kushinda mfululizo Ligi Kuu ya Englandakiwa na Chelsea na kabla ya hapo alitwaa ubingwa wa Ureno, akiwa na Porto mara mbili, na hapo ni mbali na mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Maorinho anasema hayo, wakati Real Madrid inaanza msimu wa 2012-13 kwa kumenyana na Barcelona katika Super Cup ya Hispania, Agosti 23, mwaka huu.
Mourinho akishangilia La Liga na Madrid


.png)
0 comments:
Post a Comment