Tetesi za J'tatu magazeti Ulaya
WIGAN KUMSAJILI MIYAICHI WA ARSENAL AZIBE PENGO LA VICTOR MOSES
Wigan inakamilisha dili la kumchukua kwa mkopo mchezaji wa Arsenal, Ryo Miyaichi, mwenye umri wa miaka 19, ili azibe pengo la Victor Moses, mwenye umri wa miaka 21, ambaye anatarajiwa kuhamia Chelsea.
Kocha wa Fulham, Martin Jol amemfanya usajili wa kushangaza wa Pauni Milioni 3kwa mshambuliaji wa Kifaransa, David Ngog, mwenye umri wa miaka 23, kutoka Bolton iliyoshuka daraja.
Yann M'Vila, mwenye umri wa miaka 22, amepata ofa kutoka klabu za England, Mwenyekiti wa klabu yake, Rennes amethibitisha, wakati tetesi zinasema anakwendaTottenham.
Newcastle imefikia makubaliano na Ajax ya pauni Milioni 6.2 kwa mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi, Vurnon Anita, mwenye umri wa miaka 23.
Arsenal inaweza kubadilishana mchezaji wake Nicklas Bendtner, mwenye umri wa miaka 24, na beki wa AC Milan, Philippe Mexes, mwenye umri wa miaka 30.
Akiwa amemsajili Jack Rodwell kutoka Everton, Roberto Mancini anatarajiwa kupiga hatua zaidi kwa kumsaini beki wa Liverpool, Daniel Agger wiki hii baada ya kusema anahitaji wachezaji zaidi.
Arsenal imeiambia Barcelona wanamtaka kinda Cristian Tello kama sehemu ya dili la kuwauzia Alex Song ahamie Nou Camp.
Mchezaji anayetakiwa na Newcastle, Mathieu Debuchy ameiambia klabu hiyo ifanye haraka kumsajili, kwani anataka kuondoka Lille.
BIFU KOLO TOURE NA MANCINI
Kolo Toure inadaiwa amekorofishana na kocha Mancini, baada ya kuwekwa benchi katika mechi ya Ngao ya Jamii jana ambayo Manchester City iliitwaa kwa kuifunga Chelsea 3-2.


.png)
0 comments:
Post a Comment