MSHAMBULIAJI Andy Carroll amemkumbusha uwezo wake kocha Brendan Rodgers anayetaka kumuuza, baada ya kufanya mavituz katika mechi ya mwisho ya Liverpool ya kujiandaa na msimu mpya.
Mshambuliaji huyo wa England, ambaye mustakabli wake umekuwa haueleweki katika dirisha hili la usajili, aliingia akitokea benchi kipindi cha pili na kutoa mchango mzuri akifunga bao kwa shuti la mita 20 dakika ya 66 na kuifanya Liverpool iongoze 3-0.
Ingawa Sidney Sam alipunguza bao moja kwa Bayer Leverkusen, Liverpool haikuwa kwenye hatari yoyote katika siku ambayo Raheem Sterling alicheza na kufunga bao la kwanza kabla ya Lucas Leiva kufunga na pili.
Andy Carroll anafunga
Nyumbani tena: Sami Hyypia amerejea Anfield kama kocha wa Bayer Leverkusen
Lucas Leiva akishangilia
Raheem Sterling akishangilia baada ya kufunga la kwanza


.png)
0 comments:
Post a Comment