BEKI wa Chelsea, Branislav Ivanovic
hatapewa adhabu yoyote ya kukosa mechi licha ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu jana katika mechi ya Ngao ya Jamii waliyofungwa na Man City.
Mserbia huyo alitolewa nje mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya kumchezea rafu mwananchi mwenzake, Aleksandar Kolarov na
refa Kevin Friend akamlimla nyekudu ya papo kwa papo.
Iliripotiwa kwamba Ivanovic atafungiwa mechi tatu, kuanzia mechi ya ufunguzi ya Chelsea ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Wigan Jumapili ijayo, pamoja na hayo mabadiliko ya sheria za FA Agosti mwaka 2009, yanayosema kadi nyekundu katika mechi za kujiandaa na msimu mpya haitamzuia mchezaji kucheza mechi za mashindano ndio yanamnusuru.
Kwa mabadiliko hayo ya sheria yanayohusu mechi zote zisizo za mashindano za kujiandaa na msimu mpya,
ikiwemo mechi ya Community Shield, inamaanisha Ivanovic atakuwa huru kucheza Uwanja wa DW.
KADI NYEKUNDU: Ivanovic akitolewa nje na Kevin Friend
RAFU YENYEWE: Kolarov akiangushwa chini na Ivanovic


.png)
0 comments:
Post a Comment