![]() |
| Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji kulia, akimpongeza 'Mpiganaji' Abdallah Ahmad Bin Kleb kushoto |
Na Mahmoud Zubeiry
![]() |
| Okwi |
KLABU ya Yanga tayari imeanza mazungumzo na mshambuliaji wa Simba SC, Emmanual Okwi na vyanzo vinasema ameomba mshahara wa dola za Kimarekani 3,000 kwa mwezi ili asaini klabu hiyo, ingawa haijulikani kuhusu mkataba wake wa sasa na klabu yake, Simba SC.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb yupo mjini Kampala, Uganda akishughulikia suala la mchezaji huyo wa kimataifa wa Uganda.
Jana Bin Kleb aliihakikishia BIN ZUBEIRY kwamba yupo Uganda, akisema; “Ndio, nipo Uganda, nipo Kampala hivi sasa, nakubali Rage (Ismail Aden, Mwenyekiti wa Simba), alinizidi maarifa Kigali (Rwanda) katika usajili wa Mbuyu Twite, ila sasa na mimi nataka kulipa kisasi, we subiri tu muda si mrefu utapata habari,”alisema Bin Kleb, alipozungumza na BIN ZUBEIRY kwa simu jana kutoka Kampala.
Alipoulizwa ni kuhusu mchezaji gani, Bin Kleb alikataa kumtaja, lakini BIN ZUBEIRY inafahamu kwa sasa hakuna mchezaji ambaye Simba wanamfuatilia Uganda, zaidi ya mchezaji wao tu, Okwi ambaye alikuwa Ulaya kwa majaribio ambako amefeli.
Alfajiri ya leo, BIN ZUBEIRY imewasiliana na mwandishi mmoja wa habari za michezo na burudani nchini Uganda, ambaye amesema kiongozi wa Yanga aliyekwenda Uganda amefanikiwa kumpata Okwi na wameanza mazungumzo.
“Nasikia Okwi anataka mshahara wa dola 3,000 na anataka alipwe mshahara wake wote wa mwaka, aweke benki yeye awe anafanya kazi tu,”aliusemaq mwandishi huyo wa Uganda.
Okwi amerejea wiki iliyopita Uganda, baada ya takriban wiki tatu za kuwa majaribio katika klabu ya FC Red Bull Salzburg ya Wals-Siezenheim, Austria ambayo hivyo haitamnunua.
Simba ilikuwa ina matumaini ya kupata Euro 600,000 ambazo klabu hiyo, ilikuwa tayari kutoa iwapo Mganda huyo angefuzu majaribio.
Awali, Simba ilipata ofa ya kumuuza Okwi kwa Sh. Bilioni 2 kwa klabu ya Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini, lakini mshambuliaji huyo akasema anataka kwenda Ulaya.
Awali Olando Pirates ya Afrika Kusini ilimuomba Okwi akafanye majaribio huko kama angefuzu wangemsajili dau la dola 550,000 kabla ya kuibuka kwa taarifa za kutakiwa Italia na klabu ya Parma.




.png)
0 comments:
Post a Comment