• HABARI MPYA

    Friday, January 11, 2013

    KALI ASEMA KOMBE MAPINDUZI NI LA AZAM

    Kali Ongala

    Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
    KALI Ongala, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kwamba wana matumaini ya kubeba Kombe la Tusker kesho, ingawa anakiri utakuwa mtihani mzito kwa sababu wapinzani wao, Tusker FC ya Kenya ni timu nzuri.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo, Kali alisema kwamba Wakenya wanawazidi Watanzania mambo mengi sana kisoka, lakini kwa hali yoyote Azam itapambana kubakisha taji nyumbani.
    “Itakuwa mechi ngumu, kama ulivyoiona Tusker ni timu nzuri kwa kweli, imekamilika kila idara, lakini sisi pia tuna timu nzuri na tutapigana kufa na kupona kesho,”alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga SC.
    Pamoja na hayo, Kali ameomba wapenzi wa soka Zanzibar kujitokeza kwa wingi kesho uwanjani kuishangilia Azam FC kwa sababu ni timu ya nyumbani, ili iweze kubakiza taji hilo.
    “Sisi ni timu ya Tanzania, na Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, hivyo tunaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kutushangilia ili tuweze kubakiza taji hapa nyumbani,”alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KALI ASEMA KOMBE MAPINDUZI NI LA AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top