MSHAMBULIAJI Lionel Messi usiku huu ametokea benchi na kuisaidia Barcelona kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kutoa sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Camp Nou na PSG.





Nyota huyo Argentina, aliyekuwa anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja aliingia kuchukua nafasi ya Cesc Fabregas zikiwa zimesalia dakika 28 huku wageni wakiwa wanaongoza bao 1-0 lililofungwa na Javier Pastore dakika ya 50.
Lakini Messi alichangia bao la kusawazisha la Barca lililofungwa na Pedro dakika ya 71.
David Beckham, pia alitokea benchi, akiingia zikiwa zimebaki dakika nane, lakini hakubadilisha matokeo.
Barca imefuzu kwa faida ya bao la ugenini, baada ya awali kutoa sare ya 2-2 mjini Paris katika mchezo wa kwanza.
Kikosi cha Barcelona leo kilikuwa: Valdes, Dani Alves, Pique, Adriano/Bartra dk62, Jordi Alba, Xavi, Busquets, Iniesta, Pedro, Fabregas/Messi dk62 na Villa/Song dk83.
PSG: Sirigu, Jallet/Van Der Wiel dk88, Alex, Thiago Silva, Maxwell, Lucas Moura, Verratti/Beckham dk83, Thiago Motta, Pastore, Ibrahimovic na Lavezzi/Gameiro dk 81.
Bao la kusawazisha: Pedro akiifungia Barca bao lililoipeleka Nusu Fainali
Shangwe: Gerard Pique akiungana na wachezaji wenzake wa Barcelona kushangilia bao la kusawazisha dhidi ya Paris St Germain
Super sub: Lionel Messi akiingia kuchukua nafasi ya Cesc Fabregas dakika ya 62
Anafunga: Dani Alves alishindwa kumzuia Javier Pastore na Muargentina huyo akaifungia bao la kuongoza PSG
Kitu na boksi: Victor Valdes hakuweza kuzuia mchomo wa Pastore
Halikuwa zali lao: Pastore (kushoto) akipongezwa na wenzake wa PSG baada ya kufunga Uwanja wa Nou Camp.
Mtu nyota: David Beckham akipasha kabla ya kuingia dakika ya 83
Katika mchezo mwingine, Bayern Munich ilishinda 2-0 ugenini mjini Turin dhidi ya Juventus, hivyo kufuzu kwa jumla ya mabao 4-0.
Ikichagizwa a ushindi wa awali wa mabao mawili, leo Bayern ilitakataka kutokana na mabao ya Mario Mandzukic dakika ya 64 na Claudio Pizarro dakika ya mwisho.
Ushindi huu ni mwendelezo wa furaha kwa Bayern baada ya mwishoni mwa wiki kutwaa taji la 23 la Bundesliga.
Katika mchezo huo, vikosi vilikuwa;
Juventus: Buffon, Chiellini, Barzagli, Bonucci, Pogba, Marchisio, Padoin/Isla dk69, Pirlo, Asamoah, Vucinic na Quagliarella/Matri dk66.
Bayern Munich: Neuer, Dante, Van Buyten/Boateng dk35, Lahm, Ribery, Martinez, Mueller, Alaba, Schweinsteiger, Mandzukic na Robben
Umoja: Bayern Munich wakishangilia kutinga Nusu Fainali


.png)