WACHEZAJI wa Chelsea, John Terry, Fernando Torres na David Luiz ni watu ambao huwezi kuwatambua kwa haraka wakiwa nje ya Uwanja.
Lakini wakiwa jezi zao za bluu, inakuwa rahisi kuchagua sura za wachezaji maarufu wa Chelsea.
Inhaitaji bluu? Demba Ba, Juan Mata, Fernando Torres na John Terry wakiwa pamoja katika tangazo la klabu hiyo na Adidas
Kama sehemu ya kampeni mpya ya Adidas kuzindua alama mpya ya klabu hiyo, wachezaji hao wa The Blues wametumika katika promosheni maalum.
Kama picha hizi zinavyoonyesha, wachezaji hao wapo katika mwonekano wa tofauti kama sanamu hivi.
Terry, Torres na Luiz waliungana na wachezaji wenzao Juan Mata, Demba Ba, Eden Hazard, Oscar, Gary Cahill na kipa Petr Cech katika kampeni hiyo.
Na wachezaji hao wa Chelsea walifurahia mno kushiriki kampeni hiyo kwa kupambwa rangi za klabu.
"Nimefarijika sana kuwa sehemu ya zoezi hili leo, naweza kufanya chochote kwa ajili ya klabu hii na kuonyesha mapoenzi yangu kwa kuwa bluu inamaanisha kila kitu kwangu,"alisema beki Mbrazil, David Luiz.
David Luiz, Torres na Eden Hazard ndani ya rangi za bluu
Nyota hawa tisa walikubali kupigwa picha na filamu katika zoezi lililofanyika kwenye studio za Halliford huiko Surrey - jirani na Uwanja wa mazoezi wa Chelsea, Cobham.
Zoezi lilichukua zaidi ya siku mbili Februari, kila mchezaji akitumia saa mbili akiwa amepambwa kwa rangi za bluu na glycerine ilitumika zaidi ya kuchorwa huku wakitakiwa kuweka pozi tofauti kwa ajili ya kupigwa picha.
Hapa, baadhi ya picha ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka Sportsmail juu ya zoezi hilo...
JOHN TERRY
Hii tamu: Terry akijiandaa kupakwa rangi nyingine kabla ya kupigwa picha
Ni wewe, John? Nahodha wa Chelsea katika pozi la kampeni hiyo
FERNANDO TORRES
Akipiga mpira: Torres akiwa katika pozi la picha yake
Dimbwi la bluu: Torres akifurahia kudumbukia kwenye rangi za bluu kwa ajili ya picha
Torres akipigwa picha
Magotini mwake: Tumeona ushangiliaji huu wa Torres kabla... lakini si akiwa amepakwa rangi za bluu
JUAN MATA
Hayo si maji: Mata
PETR CECH
Alama ya biashara: Petr Cech akiruka kama anafuata mpira wakati wa kupigwa picha
DAVID LUIZ
Bonge la pozi: Luiz akipigwa picha
GARY CAHILL
OSCAR
DEMBA BA
Baada ya miaka miwili ya kuvaa jezi za rangi nyeusi na nyeupe, Chelsea ilimsajili Demba Ba Januari na kuanza kuvaa jezi za bluu
Mr Manhattan: Mshambuliaji wa Senegal akionekana kama Mwanasayansi wa filamu ya Hollywood, Watchmen


.png)