KOCHA Arsene Wenger anataka kufufua makali ya Arsenal mwishoni mwa msimu kwa kumwaga kitita cha rekodi katika klabu hiyo kwenye usajili, Pauni Milioni 30 kwa kumnunua nyota wa klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani, Mario Gotze.
Wenger yu tayari kutumia jumla ya Pauni Milioni 70 kwa ajili ya usajili lakini kiwango hicho kinatakiwa pia kugharamia na mishahara ya wachezaji wapya, na kiungo huyo mshambuliaji wa Dortmund mwenye umri wa miaka 20 anatakiwa sana.
Gotze ana thamani ya Pauni Milioni 30, ambazo zinaweza kumfanya ahame klabu kama itatokea klabu ya kufika bei hiyo - na Arsenal iko tayari kufanya hivyo.
Anatakiwa: Mario Gotze akishangilia bao lake Bundesliga dhidi ya Greuther Fuerth
Ni Fabregas mpya?
Gedion Zelalem anacheza nafasi ile ile ya kiungo kama Jack Wilshere na Cesc Fabregas na anaweza kufuata nyayo hizo katika kikosi cha Arsenal, kupitia michuano ya Kombe la Ligi, Capital One.
Zelalem , mwenye miaka 16, alizaliwa Ujerumani ambako baba yake alipewa hifadhi ya ukimbizi.
Mama yake alifariki dunia mwaka 2005 na familia yake ikahamia Marekani mwaka uliofuata ambako alisoma katika shule ya Walter Johnson.
Wenger pia anataka kumsajili mchezaji mwenye thamani ya Pauni Milioni 10, kiungo wa Toulouse ya Ufaransa, Etienne Capoue na pia anataka kumsajili kipa mzoefu wa Liverpool, Pepe Reina.
Pamoja na usajili huo, bado inatarajiwa Wenger ataendelea na utamaduni wake wa kuinua vipaji vya vijana.
Gedion Zelalem, Mjerumani mwenye umri wa miaka 16 ambaye baba yake ni mkimbizi wa Ethiopia aliyepewa hifadhi Ujerumani, amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha kwanza na anatarajiwa kupandishwa kwenye kikosi hicho msimu ujao.
Hector Bellerin, beki wa kulia mwenye umri wa miaka 18 kutoka Barcelona, na Serge Gnabry, kiungo mwenye umri wa miaka 17 kutoka Stuttgart, pia wanaweza kutua Arsenal.
Lakini Zelalem, mwenye uzoefu wa kucheza soka katika vyuo vikuu Marekani, atavutia zaidi akiwa ana ndoto za kufuata nyayo za akina Cesc Fabregas na Jack Wilshere atakapoanza kuichezea Gunners katika michuano ya Kombe la Ligi, Capital One msimu ujao.
Fabregas mpya: Gedion Zelalem akiichezea timu ya vijana ya Arsenal chini ya umri wa miaka 21
Zelalem hakuwa kwenye timu yoyote wakati anachukuliwa na msaka vipaji wa Arsenal Marekani, Danny Karbassiyoon, lakini anacheza nafasi moja na Wilshere na Fabregas.
Baba yake- Zelalem Woldyes - alihamia Ujerumani ambako kijana wake huyo alizaliwa.
Pamoja na hayo, aliwahi kushiriki programu ya vijana ya klabu ya Hertha Berlin, familia yake ikahamia Washington DC mwaka 2006, ambako alikuwa akichezea chuo cha Walter Johnson hadi akaivutia Arsenal.
Mwanzo mzuri: Gedion Zelalem akiingia uwanjani
Zelalem alianza vizuri akiichezea Arsenal U-21 dhidi ya Liverpool Jumatatu. Kocha wa vijana wa Arsenal, Steve Gatting alisema: "Anakuja na vitu vingi. Ana miaka 16 tu na hiyo ilikuwa mechi yake ya kwanza kuichezea klabu katika mashindano na amefanya vizuri mno,".
Zelalem amekuwa akiitwa katika timu za vijana za Ujerumani, lakini pia amekuwa akifanya mazoezi na Marekani, ambako aliomba uraia.