• HABARI MPYA

    Thursday, May 09, 2013

    KUELEKEA TUZO ZA KILI KIKWETUKWETU 2013, NANI ANASTAHILI KURA YAKO HAPA?

    Kala Jeremiah kulia na Mwasiti kushoto; Miongoni mwa wasanii wanaowania tuzo ya wimbo bora mwaka tuzo za Kili 2013.

    Na Princess Asia
    WAKATI zoezi la upigaji wa kura za tuzo za wanamuziki bora Tanzania, maarufu kama Kilimanjaro Music Award lilianza Mei 2, mwaka huu, kipengele cha wimbo bora wa mwaka kinaonekana kuwa na upinzani mzito.
    Katika kipengele hicho, Rapa Kala Jeremiah, kupitia wimbo wake Dear God anachuana na kundi la Kigoma All Stars na wimbo wao Leka Dutigite, Mwasiti aliyemshirikisha Ally Nipishe katika wimbo Mapito, Ommy Dimpoz aliyemshirikisha Vanessa Mdee katika wimbo Me n U na Ben Pol katika wimbo Pete.
    Nyimbo zote hizo zimekuwa zikifanya vizuri kuanzia mwaka jana zikitamba hadi nje ya nchi, hususan Kenya na Uganda, nchi jirani ambazo zinafuatilia muziki wetu.
    Katika kipengele hiki, msanii atabebwa na idadi ya kura atakazopigiwa na mashabiki wake ili aweze kushinda tuzo hiyo. 
    Wapiga kura wanatakiwa kuandika namba ya msanii, wimbo, kikundi au bendi anayotaka ishinde na kisha kutuma kwenda namba 15346, wakati njia nyingine zaidi ya ujumbe mfupi (SMS) ni pamoja na Email, kwenda ktma@innovex.co.tz au kutembelea tovuti ya www.kilitimetz.com na kupiga kura moja kwa moja.
    Meneja wa Bia Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini wa tuzo hizo, George Kavishe aliiambia BIN ZUBEIRY kwamba, wamejiandaa vizuri mwaka huu kuhakikisha zoezi linafana.
    Kilele cha sherehe za utoaji tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards zilizobeba kaulimbiu ya Kikwetu kwetu ni Juni 8, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City, ambako pamoja na wasanii mbalimbali kupokea tuzo kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali pia. 
    Je, katika wimbo bora wa mwaka unampa nani kura yako?
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KUELEKEA TUZO ZA KILI KIKWETUKWETU 2013, NANI ANASTAHILI KURA YAKO HAPA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top