![]() |
Moyes baada ya kutambulishwa leo |
Na Mahmoud Zubeiry IMEWEKWA MEI 9, 2013 SAA 12:45 JIONI
KLABU ya Manchester United ya England rasmi jioni hii imemtaja David Moyes kuwa kocha wake mpya.
Kwa mujibu wa taarifa ambayo, BIN ZUBEIRY imetumiwa na Manchester Unted, Moyes ndiye mrithi wa Sir Alex Ferguson aliyejiuzulu jana baada ya miaka 27 kuitumikia klabu hiyo na ataanza kazi rasmi Julai 1, mwaka huu.
Taarifa hiyo imesema, Moyes amepewa mkataba wa miaka sita kuanzia msimu wa 2013/14.
David, mwenye umri wa miaka 50, amekuwa kocha wa Everton tangu mwaka 2002, alipojiunga nayo akitokea Preston North End alipofanya kazi kwa mafanikio.
Akimtangaza mrithi wake, Sir Alex Ferguson amesema: “Wakati tukijadili mtu ambaye atafaa, wengi tulikubaliana na David Moyes. David ni mtu mwenye upeo wa hali ya juu, anayejituma na mwadilifu. Nimekuwa nikivutiwa na kazi yake kwa muda mrefu na nilimuomba awe Msaidizi wangu mwaka 1998 hapa.
Alikuwa kijana mdogo na mwanzoni kabisa wa maisha yake ya ukocha na tangu wakati huo ameendelea kufanya kazi nzuri Everton. Hakuna swali juu ya kuwa na vigezo vyote vya kuiongoza klabu hii,”alisema.
Kwa upande wake, Sir Bobby Charlton alisema: “Wakati Wote nimekuwa nikisema kwamba kocha ajaye atakuwa mtu babu kubwa Manchester United. Kwa David Moyes, tuna mtu ambaye anatambua vitu ambavyo vinaifanya klabu hii iwe maalum,”alisema.
TAARIFA RASMI ILIYOTUMWA KWA BIN ZUBEIRY KUTOKA MAN UNITED HII HAPA;
David Moyes appointed Manager of Manchester United
|