• HABARI MPYA

    Thursday, May 09, 2013

    RONALDO ANAREJEA MAN UNITED, GILL ATUA MADRID KUZUNGUMZA NA WAKALA WAKE, ROONEY ANAONDOKA


    IMEWEKWA MEI 9, 2013. SAA 7:25 USIKU
    WAKATI Sir Alex Ferguson anaachia ngazi, mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney ameomba kuondoka pia Old Trafford wakati ambao habari zinasema klabu iko mbioni kumrejesha Cristiano Ronaldo.
    Saa kadhaa baada ya Ferguson kuthibitisha atastaafu ukocha United mwishoni mwa msimu, akimpisha kocha wa Everton, David Moyes, inabainika Rooney alimuambia Ferguson wiki mbili zilizopita anataka kuanza maisha mapya.
    Wakati huo huo, inagundulika, Mtendaji Mkuu wa United, David Gill alikuwa mjini Madrid kukutana na Jorge Mendes, wakala maarufu Mreno anayemuwakilisha Ronaldo. Vyanzo vimesema jana usiku kwamba, United inajiamini itamrejesha mchezaji huyo iliyemuuza Real Madrid kwa dau la rekodi ya dunia, Pauni Milioni 80, mwaka 2009. 
    The way they were: Rooney and Ronaldo shone together for Man United
    Jinsi walivyokuwa: Wayne Rooney na Cristiano Ronaldo wakati wanacheza pamoja Manchester United
    Once a Blue: Chelsea are confident of luring the £25m England international to Stamford Bridge in the summer
    Katika bluu: Chelsea ina matumaini ya kumnasa mshambuliaji huyo wa England kwa Pauni Milioni 25 ahamie Stamford Bridge msimu ujao
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: RONALDO ANAREJEA MAN UNITED, GILL ATUA MADRID KUZUNGUMZA NA WAKALA WAKE, ROONEY ANAONDOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top