• HABARI MPYA

    Friday, May 10, 2013

    WAZEE YANGA WAMSHUSHIA PONGEZI NZITO MANJI NA JESHI LAKE LA MIAMVULI KWA UBINGWA

    Manji

    IMWEKWA MEI 10, 2013 SAA 7:53
    “Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Wazee wa YANGA, Napenda Kuwafahamisha kuwa Wazee wa YANGA wamefurahi na kuwashukuru Viongozi wa Klabu ya YANGA chini ya Mwenyekiti Yusuf Manji na Makamu Mwenyekiti Clement Sanga kwa kuongoza Klabu na kuweza kunyakua Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu wa mwaka 2012/2013. Ushindi huu umetokana na Uongozi bora, uwajibikaji katika kutekeleza majukumu ya Klabu na kufikia malengo.
    Mwenyekiti wetu ametujengea dhana ya kuwa na imani ndani ya Uongozi, wanachama na wachezaji wetu.
    Hivyo basi na sisi kama wazee wa Klabu tunayo imani na viongozi na wachezaji wetu na tunaahidi kuwa mchezo wetu wa tarehe 18 Mei 2013 kati yetu na Simba lazima tushinde ili tusherehekee Ubingwa wetu kwa furaha, shangwe na nderemo.

    “YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO”
    K.n.y: YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB na 
    MWENYEKITI WA WAZEE YANGA ALHAJ JABIRI M. KATUNDU
    Naomba kuwasilisha.
    IBRAHIM O. AKILIMALI
    KATIBU WA WAZEE WA YANGA,”.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: WAZEE YANGA WAMSHUSHIA PONGEZI NZITO MANJI NA JESHI LAKE LA MIAMVULI KWA UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top