IMEWEKWA JUNI 6, 2013 SAA 6:12 USIKU
KIUNGO Mbrazil, Fernandinho amewasili Kaskazini magharibi kwa ajili ya vipimo vya afya baada ya Shakhtar Donetsk kukubali ofa ya Pauni Milioni 22 kutoka Manchester City.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye ametaka kuhamia Ligi Kuu England ili kuongeza matumaini ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia Brazil mwakani, alipigwa picha katika hospitali ya Bridgewater, Manchester.
Fernandinho alikuwa ana wasiwasi ndoto zake za kucheza England zingezimwa na klabu yake, Shakhtar.
Fernandinho akiwasili kwa ajili ya vipimo katika hospitali ya Manchester hospital
UKO WAPI UDHAIFU NA UBORA WA FERNANDINHO?
Fernandinho ni mpitiaji hodari wa mipira miguuni mwa wapinzani, mwenye kasi na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira. Anacheza vizuri katika ulinzi, lakini pia ni hodari mno katika kuichezesha timu.
Si kwamba ana kipaji halisi kama cha Andrea Pirlo, bali ni mzuri katika kumiliki mpira, ana mbinu na maarifa sambamba na hesabu kali kuanzia katika ulinzi hadi kushambulia.
Mtu ambaye unaweza kumfananisha naye kwa haraka katika soka ya England anaweza kuwa mchezaji wa Chelsea, Mbrazil pia, Ramires, lakini pasi za Fernandinho ni za hatari zaidi kuliko za mwenzake huyo.