• HABARI MPYA

    Friday, June 07, 2013

    MOURINHO AHAHA KUINASA SAINI YA MPACHIKA MABAO WA BRAZIL HULK

    IMEWEKWA JUNI 7, 2013 SAA 7:00 USIKU
    MSHAMBULIAJI wa Brazil, Hulk amethibitisha Jose Mourinho anamtaka Stamford Bridge na ametoa ofa ya Pauni Milioni 35 kumng'oa Zenit St Petersburg.
    Zenit kwa sasa imeichunia ofa ya Chelsea na wanataka kiasi cha karibu Pauni Milioni 50 walizolipa kwa Porto kumpata mshambuliaji huyo mwenye kasi msimu uliopita.
    Hulk anataka kuondoka Urusi na anahusishwa na kuungana na Mourinho na aliweka wazi hilo mbele ya Waandishi wa Habari kwamba anajua Chelsea wametoa ofa kwa ajili yake.
    Wanted man: Hulk (right) is being targeted by new Chelsea manager Jose Mourinho
    Anayetakiwa: Hulk (kulia) anatakiwa na kocha mpya wa Chelsea, Jose Mourinho

    Alipoulizwa kuhusu hilo na Waandishi nchini Brazil jana mchana, alijibu: "Ikiwa nitasema hakukuwa na kitu juu ya hili, nitakuwa nadanganya. Lakini hiyo si kwa sasa. Kwa sasa, Kwa asilimia 100 akili yangu nimeielekeza Selecao (Kireno, maana yake timu ya taifa ya Brazil), na natumaini nitakuwepo na kushinda na timu yangu kwenye Kombe la Mabara.
    "Ni jambo la kujivunia mno kwangu kucheza nimevaa jezi za njano, karibu mno na familia yangu. Matatizo mengine itabidi yasubiri hadi wakati wake utakapofika.’
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MOURINHO AHAHA KUINASA SAINI YA MPACHIKA MABAO WA BRAZIL HULK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top