• HABARI MPYA

    Wednesday, July 10, 2013

    FRIENDS RANGERS NA POLISI JAMII KUCHEZA UWANJA ALIOUFUNGUA RAIS JK JUMAPILI

    Uwanja wa Azam ulizinduliwa na JK; Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete akifungua jiwe la Msingi la Uwanja wa Azam Complex hivi karibuni. Uwanja huo utatumika kwa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa
    Na Boniface Wambura, IMEWEKWA JULAI 10, 2013 SAA 10:51 JIONI
    MECHI ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kati ya Friends Rangers ya Dar es Salaam na Polisi Jamii ya Mara iliyokuwa ichezwe Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) imesogezwa mbele kwa siku moja.
    Timu hizo sasa zitacheza Jumapili (Julai 14 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi. Polisi Jamii ilishinda bao 1-0 mechi ya kwanza iliyochezwa Julai 6 mwaka huu Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
    Refa Hans Mabena kutoka Tanga ndiye atakayechezesha mechi akisaidiwa na E. Mkumbukwa na Hajj Mwalukuta wote kutoka Tanga. Mwamuzi wa akiba (fourth official) ni Kessy Ngao wa Dar es Salaam.
    Mechi kati ya Stand United FC ya Shinyanga na Kimondo SC ya Mbeya itachezwa Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Mwamuzi atakuwa Daniel Warioba kutoka Mwanza. Kimondo SC ilishinda mechi ya kwanza bao 1-0.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: FRIENDS RANGERS NA POLISI JAMII KUCHEZA UWANJA ALIOUFUNGUA RAIS JK JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top