• HABARI MPYA

    Wednesday, July 10, 2013

    MTOTO WA ANDY COLE AJUMUISHWA KIKOSI CHA KWANZA MAN CITY KWA ZIARA YA KUJIANDAA NA MSIMU MPYA AFRIKA KUSINI

    IMEWEKWA JULAI 10, 2013 SAA 11:30 JIONI
    KOCHA Manuel Pellegrini amemuorodhesha Devante Cole katika kikosi chake cha Manchester City kwa ajili ya ziara ya kujiandaa na msimu mpya Afrika Kusini. 
    Kinda huyo nyota wa City ni mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa England na mahasimu wao, Man United, Andy Cole na amekuwa akichezea timu ya akademi ya Etihad.
    Like father, like son: Devante Cole in action for Manchester City
    Kama baba, kama mwana: Devante Cole akiichezea Manchester City

    Cole mdogo mwenye umri wa miaka 18, amefuata karibu kila kitu kwa baba yake kichezaji – wepesi na kasi, uchezaji, namna anavyopambana uwanjani na jinsi anavyolijua goli.
    Pellegrini atakipeleka kikosi chake kipya huko katika ziara ya mechi mbili Afrika Kusini kuanzia Julai 14 dhidi ya Supersport mjini Pretoria na kisha AmaZulu mjini Durban siku nne baadaye.  
    Cole the goal: Devante is following in the footsteps of his father Andy who played for Manchester City
    Cole Mabao: Devante anafuata nyayo za baba yake, Andy ambaye alichezea Manchester City pia
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MTOTO WA ANDY COLE AJUMUISHWA KIKOSI CHA KWANZA MAN CITY KWA ZIARA YA KUJIANDAA NA MSIMU MPYA AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top