IMEWEKWA JULAI 10, 2013 SAA 11:50 ALFAJIRI
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga jana alikutana na Wahariri wa Habari za Michezo wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, makao makuu ya shirikisho hilo, Uwanja wa Karume, Ilala mjini Dar es Salaam.
Kinachoonekana lengo la Tenga kukutana na Wahariri hao ni kuweka sawa mazingira anayoyataka kuelekea kwenye Mkutano Mkuu wa Dharula wa shirikisho hilo Jumamosi mjini Dar es Salaam, kujadili marekebisho ya Katiba.
Beki huyo wa zamani wa Yanga SC, Pan Africans na timu ya taifa, Tenga alisema hakuna hila zozote katika mchakato wa marekebisho ya Katiba, kwa vile yametokana na maagizo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Rais Tenga amewahakikishia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Dharura kuwa dhamira ya marekebisho hayo ni nzuri, kwani lengo ni kila mtu apate haki yake.
Amesema Mkutano huo utakaofanyika Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) utakuwa na ajenda moja tu ya kuingiza Kamati ya Maadili, na Kamati ya Rufani ya Maadili katika Katiba ya TFF kama ilivyoelekezwa na FIFA ili baadaye uanze mchakato wa uchaguzi.
“Katika kuunda Kamati ya Maadili tumeangalia ile ile ya FIFA, tusitengeneze kitu kipya, yaondolewe yale yanayotakiwa kuondolewa, na yaongezwe yale yanayotakiwa kuongozwa. Kwa sababu tumeangalia mazingira kwa Tanzania ni tofauti na Ujerumani au nchi za sehemu nyingine,” alisema.
Rais Tenga amewataka wajumbe wafike kwenye Mkutano wakiwa na mtazamo wa kujenga, kwani kuna maagizo ya FIFA ambayo wanatakiwa kuyatekeleza ili wasonge mbele.
“Tutawaeleza kwanini hili limewekwa na lile limeondolewa. Mpira unataka unit (kitu kimoja), ni mchezo wa kila mtu. Baada ya hapa tunaanzisha mchakato wa uchaguzi. Watu wanaingia wakiwa wamoja, wanatoa hoja wanasikilizwa. Wanahukumiwa kwa hoja,” alisema na kuongeza utatolewa muda wa kutosha wajumbe ili wayaone na kuelewa marekebisho hayo.
Hapa Tenga alikuwa anatengeneza mazingira ya Mkutano mwepesi Jumamosi, lakini pamoja na ‘siasa’ hizo za soka, beki huyo wa kikosi cha Taifa Stars kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 1980 Lagos, kuna jambo la msingi alizungumza jana.
Tenga alisema katika kipindi hiki cha usajili, vema klabu zikawaachia wataalamu wa mpira wa miguu kufanya kazi hiyo, kwani ndiyo wanaojua upungufu wa timu, hivyo wanaweza kusajili wachezaji sahihi.
Amesema tatizo kubwa la klabu za Tanzania ni kuwa, timu zao hazina uwezo wa kuhimili dakika 90 na kwa sababu hiyo, watu wanapaswa pia kuzungumzia aina ya mazoezi ambayo timu zao zinafanya badala ya kubakia kutaja tu majina ya wachezaji wanaotaka kusajiliwa.
Tenga pamoja na kuwa Mhandisi wa kiwango cha juu na mwanasoka nguli mstaafu, lakini pia ni kocha wa mpira wa miguu tena wa daraja la kwanza nchini na alichokizungumza ni ukweli kabisa, ila tu inasikitisha hakukijadili kwa mapana marefu.
Hii ndiyo aina ya mijadala inayopaswa kuanzishwa na watu kama Tenga wenye heshima yao kubwa linapokuja suala la soka kitaalamu. Anaijua kwa kuicheza na kwa kuisomea kama mtaalamu, yaani mwalimu.
Lakini pia ana uzoefu wa soka ya Tanzania kuanzia kuwa mchezaji, kocha hadi kiongozi. Amezungumza kitu sahihi hakuna shaka.
Yanga SC baada ya msimu tu, kocha wao Ernie Brandts alipanda ndege kurejea kwao Uholanzi- na huku nyuma pilika za usajili zikaanza. Ukiwauliza viongozi, wanasema kocha katika ripoti yake, aliacha maagizo wachezaji fulani waachwe, na wachezaji wa nafasi fulani wasajiliwe.
Jamani, hivi kweli Brandts beki wa zamani wa Uholanzi aliyecheza hadi Fainali za Kombe la Dunia na mwalimu aliyepewa leseni ya daraja la kwanza ya kufundisha soka na Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), anaweza kufanya hivi?
Anaagiza aondolewe kikosini mchezaji ambaye anamjua na amekaa naye kwa msimu mzima, halafu anaagiza asajiliwe mchezaji asiyemjua kabisa, ili mradi awe anacheza nafasi anayotaka ipatiwe mchezaji mpya.
Hakuna kitu hicho- na wala Brandts hawezi hata siku moja kupingana na viongozi wa Yanga, kwa sababu anajua akifanya hivyo dakika chache baadaye atapewa tiketi ya kurejea kwao kama ilivyokuwa kwa Mbelgiji, Tom Saintfiet aliyemtangulia.
Lakini hii ndiyo desturi ya hata kwa mahasimu wao, Simba SC, viongozi ndiyo wansajili na si kocha. Msimu umeisha kocha Mfaransa Patrick Liewig ametupiwa virago kaajiriwa kocha mpya, Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ anakuta tayari usajili umekwishafanyika kwa asilimia kubwa.
Wa kuachwa wameachwa, wa kusajiliwa wamesajiliwa, sasa jiulize kwa jinsi hii mwisho wa msimu timu ikifanya vibaya na ikathibitika chanzo ni wachezaji wasio na viwango, nani wa kubeba lawama?
Lakini kwa vyovyote atakayetolewa kafara ni Kibadeni tu, japokuwa ukweli ni kwamba aliyesajili ndiye anapaswa kubeba mzigo wa lawama.
Kama alivyosema Tenga, lazima ufike wakati Simba na Yanga zibadilike na zichague kujiendesha kitaalamu badala ya mfumo wa kimachinga na kimagumashi huu tunaoushuhudia sasa.
Angalia Azam pale, huhitaji kudadisi kujua kama Stewart Hall ndiye mwenye mamlaka ya usajili- msimu umeisha ameangalia wachezaji ambao wanastahili kuondoka iwe moja kwa moja au kwa mkopo, amewaonyesha njia.
Lakini kuhusu kuongeza watu, amekataa na amesema kama kufanya hivyo ni hadi mwishoni mwa mwaka baada ya kuitathmini timu katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, kwa sababu kipindi hicho ndipo atakuwa anafanya usajili mkubwa pia kwa ajili ya michuano ya Afrika.
Hiyo ni timu ambayo imemaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu na kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ilifika hatua ya 16 Bora, kocha wake ameona iko vizuri tu na kama marekebisho ni baada ya kukitathmini tena kikosi kwa miezi kadhaa ijayo.
Yanga kuna mtu amekwishafika hadi Vietnam kufuata saini ya Moses Olyola, wachezaji kama 10 hivi wapya wamekwishasajiliwa- na hiyo ndiyo timu iliyomaliza msimu vizuri ikitwaa ubingwa na kuzifunga timu zote pinzani, Azam na Simba.
Unaweza kustaajabu mashabiki wa Yanga wanajua soka kuliko viongozi wao- kwa sababu baada ya msimu, wana Yanga wote walikuwa wanazungumza lugha moja, wanahitaji mshambuliaji mmoja wa kiwango cha juu kuliko waliopo sasa kwenye timu, zaidi ya hapo timu imekamilika kila idara.
Kuna mchezaji kasajiliwa Yanga kwa sababu alikwenda kwenye majaribio Msumbiji na ametokea kwenye kituo ambacho ametokea pia Mbwana Samatta, anaitwa Shaaban Kondo. Kwa mtaji huu, Barcelona ingesajili wote wa akademi ya ASEC kwa kujua watampata Yaya Toure mwingine.
Wakati fulani alisajiliwa mchezaji Yanga eti kwa sababu alikwenda kufanya majaribio akademi ya Arsenal, lakini baada ya wenyewe kugundua ni galasa wakamuacha bila kutoa taarifa wala picha kwenye magazeti. Ile kimya kimya.
Lakini kama alivyosema Tenga, iwapo mambo ya usajili wangeachiwa wataalamu wayafanye, hasara na fedheha kama hizi zingeepukwa. Ramadhan Kareem.