• HABARI MPYA

    Sunday, August 18, 2013

    ABRAMOVICH AVUNJA UKIMYA NA KUFUNGUKA CHELSEA...AMETUMIA PAUNI MILIONI 713 KUNUNUA WACHEZAJI 72, MAFANIKIO YAKE NI...

    IMEWEKWA AGOSTI 18, 2013 SAA 12:10 JIONI
    MMILIKI wa Chelsea, Roman Abramovich, ambaye amekuwa hatokeo kuzungumza katika umma au kwenye Vyombo vya Habari, amevunja ukimya wake kwa kwa kutoa shukrani kwa mashabiki wa Chelsea kwa sapoti waliyompa kwa muongo mzima wa kumiliki timu hiyo.
    Bilionea huyo Mrusi, ambaye aliichukua timu hiyo Julai mwaka 2003, ameandika ujumbe katika bango la ratiba za mechi kuelekea mchezo wa nyumnani na Hull.
    Inasomeka: "Tumekuwa na muongo mzuri pamoja na klabu isingefikia mafanikio haya bila nyinyi. Nawashukuru kwa sapoti, kuna miaka zaidi ya mafanikio.'
    Nenda chini kuangalia ukurasa wa ujumbe huo
    Happy times: Roman Abramovich lifted the Champions League with Chelsea in 2012
    Wakati wa furaha: Roman Abramovich akiinua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya la Chelsea mwaka 2012
    A decade of success: Abramovich has helped create a side that has become used to winning silverware
    Muongo wa mafanikio: Abramovich amesaidia kujenga kikosi cha ushindi

    Tangu kuwasili kwa Abramovich, klabu hiyo imepitia kwenye mafanikio ambayo haijawahi kupata kabla.
    Pamoja na mataji matatu ya Ligi Kuu England, Chelsea pia imetwaa mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, UEFA ndogo maarufu kama Europa League, na Kombe la FA mara nne na Kombe la Ligi mara mbili.
    Katika kipindi hicho, ametumia kiasi cha Pauni Milioni 713 kununua wachezaji 72
    Roman's message
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ABRAMOVICH AVUNJA UKIMYA NA KUFUNGUKA CHELSEA...AMETUMIA PAUNI MILIONI 713 KUNUNUA WACHEZAJI 72, MAFANIKIO YAKE NI... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top