• HABARI MPYA

    Friday, May 16, 2014

    HIVI NDIVYO MESSI ALIVYOMDONDOSHA RONALDO KIMASLAHI

    MSHAMBULIAJI Lionel Messi atakuwa akilipwa Pauni Milioni 16.3 kwa mwaka katika mkataba mpya aliokubali kusaini na klabu yake, Barcelona mambo ambalo litamfanya Muargentina huyo awe mwanasoka anayelipwa zaidi duniani. 
    Baba wa mchezaji huyo Jorge alikutana na viongozi wa klabu hiyo Javier Faus na Antoni Rossich wiki iliyopita na kufikia makubaliano ya mkataba wa saba ndani ya miaka 11 ya mshindi huyo wa Ballon d’Or nne Barcelona. 
    Messi atafikisha miaka 27 June na mkataba mpya unatarajiwa kuweka Camp Nou hadi mwaka 2018.
    Kwa mshahara huo mpya, Messi anampiku hasimu wake, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ambaye analipwa Pauni Milioni 15 kwa mwaka.  
    Milionea: Messi amekubali kusaini mkataba mpya Barcelona ambao utamfanya awe mwanasoka anayelipwa zaidi ya wote duniani
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HIVI NDIVYO MESSI ALIVYOMDONDOSHA RONALDO KIMASLAHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top