• HABARI MPYA

    Wednesday, November 05, 2014

    LIVERPOOL YAIPIA 1-0 YA 'KISHIKAJI' LIVERPOOL CHOVU CHOVU LIGI YA MABINGWA

    BAO pekee la Karim Benzema usiku huu limeipa ushindi wa 1-0 Real Madrid katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool, Uwanja wa Bernabeu, Madrid.
    Mfaransa huyo alifunga bao hilo dakika ya 27 katika mchezo ambao, kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers aliwapumzisha wachezaji wake saba wa kikosi cha kwanza, akiwemo Nahodha Steven Gerrard na mshambuliaji Mario Balotelli
    Gerrard na Raheem Sterling walitokea benchi dakika ya 69 kwenye mchezo huo, ambao Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo alipoteza nafasi kadhaa za kufunga.
    Ushindi huo, unaifanya Real itimize pointi 12 baada ya kucheza mechi nne na kushinda zote, ikifuatiwa na FC Basel yenye pointi sita, Liverpool tatu sawa na Ludogorets Razgrad, zote pia zimecheza mechi nne kila moja. 
    Mchezo mwingine wa kundi hilo usiku huu, FC Basel imeshinda 4-0 dhidi ya  Ludogorets Razgrad, mabao ya Breel Embolo dakika ya 34, Derlis Gonzalez dakika ya 41, Shkelzen Gashi dakika ya 59 na Marek Suchy dakika ya 65.
    Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Arbeloa/Nacho dk83, Varane, Ramos, Marcelo, Modric, Kroos, Isco, Rodriguez/Bale dk62, Ronaldo na Benzema/Hernandez dk87.
    Liverpool; Mignolet, Manquillo, Toure, Skrtel, Moreno, Can/Coutinho dk75, Lucas/Gerrard dk69, Lallana, Allen, Markovic/Sterling dk69 na Borini.
    Karim Benzema (wa pili kushoto) akipasua katikati ya wachezaji wa Liverpool, Alberto Moreno (kushoto) na Joe Allen na Adam Lallana (kulia) 

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2820851/Real-Madrid-1-0-Liverpool-Karim-Benzema-poaches-winner-hosts-Brendan-Rodgers-reserves-avoid-pain-Spain.html#ixzz3I8leXggr
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIVERPOOL YAIPIA 1-0 YA 'KISHIKAJI' LIVERPOOL CHOVU CHOVU LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top