• HABARI MPYA

    Saturday, March 21, 2026

    YANGA SC YATOA SARE NYINGINE, 1-1 NA MTIBWA DODOMA


    MABINGWA watetezi, Yanga SC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
    Yanga walitangulia kwa bao la kiungo Muiovory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua dakika ya 23, kabla ya kiungo Ismail Aidan Mhesa kusawazisha kwa kona aliyopiga ikaingia moja kwa moja nyavuni dakika ya 90’+2.
    Kwa matokeo hayo, Yanga SC inafikisha pointi 38 katika mchezo wa 16 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 10 zaidi ya watani wao, Simba SC walio nafasi ya tatu ambao hata hivyo wana mechi tatu mkononi.
    Katikati ya Simba na Yanga wapo Azam FC nafasi ya pili wakiwa na pointi 29 baada ya kucheza mechi 15.
    Kwa sare ya leo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 22 katika mchezo wa 17 na kusogea nafasi ya saba. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YATOA SARE NYINGINE, 1-1 NA MTIBWA DODOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top