MFANYABIASHARA na Mwanasiasa maarufu Hispania, Joan Laporta i Estruch ataendelea kuwa Rais wa klabu ya FC Barcelona kwa awamu ya nne.
Hiyo ni baada ya jana kuchguliwa tena katika uchaguzi uliofanyika akipata kura 32,934, sawa na asilimia 68.18% ya kura zote na kumuangusha mpinzani wake mkuu, Víctor Font i Manté ambaye ni Mfanyabiashara mkubwa Katalunya aliyepata kura 14,385 sawa na asilimia 29.78 huku kura nyingine 984 sawa na asilimia 2.04 zikiharibika.
Joan Laporta amekuwa Rais wa klabu hiyo kuanzia mwaka 2003 hadi 2010 na tena kuanzia Machi 2021 aliposhinda kwa kura 30,184 sawa na asilimia 54.28%.
Miaka mitano tangu uchaguzi uliopita, kura za Joan Laporta – mwanachama mwenye kadi namba 9,601 Barca ameshinda tena kwa kishindo.
Joan Laporta alizaliwa Juni 29 mwaka 1962 huko huko Barcelona na ndiye Rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia FC Barcelona kuongoza Klabu hiyo katika vipindi viwili tofauti.
Akiwa amehitimu katika Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Barcelona, pia ana Shahada ya Uzamili ya Sheria Kodi kutoka Taasisi ya Estudios Superiores Abat Oliba huko huko Barcelona.
Yeye ni mshirika mwanzilishi na mmiliki wa kampuni ya kisheria ya Laporta & Arbós Advocats Associates; mwanachama wa Chama cha Wanasheria cha Barcelona na, miongoni mwa nafasi zingine, ni mlezi na mwanachama wa tume ya Utendaji ya Lluch Foundation na mlezi wa Johan Cruyff Welfare Foundation.



.png)
0 comments:
Post a Comment