• HABARI MPYA

    Saturday, July 14, 2012

    SIMBA WAFIKIRIA KUJITOA KAGAME

    Yondan anasaini Yanga na mpunga mezani huo

    Na Mahmoud Zubeiry
    HIVI unaposoma habari hii, Simba SC wapo kwenye kikao, kujadili juu ya uamuzi wa kushiriki au kutoshiriki mchuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame, iliyoanza leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
    Kisa nini? Hawana imani na wenyeji wa michuano hiyo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pamoja na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECFA). Kivipi? Ni kutokana na kiteno cha vyombo hivyo kumpa leseni beki wao, Kelvin Patrick Yondan achezee Yanga SC, ambao ni wapinzani wao wa jadi.
    Habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka ndani ya Simba SC, zimesema kwamba kitendo cha Yanga kumchezesha Yondan kwenye klabu hiyo leo, katika mchezo dhidi ya Atletico ya Burundi, kimeikera sana Simba na kinahisi kuna hujuma wanafanyiwa na TFF na CECAFA.
    Ikumbukwe Yondan aliyejiunga na Simba 2006, alijiunga na Yanga mwezi uliopita ingawa klabu yake inaendelea kudai, ina mkataba naye.
    BIN ZUBEIRY ilifanikiwa kuwa chombo cha kwanza cha habari duniani kuonyesha mikataba yote ya Simba na Yanga dhidi ya Yondan.
    Lakini Yondan, beki wa kati hodari nchini, mwenyewe hajawahi hata siku moja kuukana mkataba wowote kati ya hiyo, zaidi ya kusema kujiunga kwake na Yanga, Simba watajijua wenyewe.
    Mwishoni mwa mwaka jana, Yondan alisusa kuchezea Simba na kuamua kubaki kwao mjini Mwanza, baada ya mechi dhidi Toto African ya mini humo ya Ligi Kuu.
    Na ndipo hapo zilipoanza kuibuka habari za mchezaji huyo kuhamia kwa watani wa jadi, hadi Mei mwaka huu alipomwaga wino Jangwani.
    Ingawa Yondan kwa sasa yupo kwenye kambi ya timu mpya, Yanga, lakini klabu yake Simba SC imeendelea kusistiza huyo ni mchezaji wao halali na sasa inafikiria kujitoa kwenye Kagame baada ya Vidic wa Tanzania kuchezea Yanga kwenye michuano hiyo.    
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA WAFIKIRIA KUJITOA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top