• HABARI MPYA

    Tuesday, July 09, 2013

    MOYES AANZA ZAMA MPYA MAN UNITED...WACHEZAJI WOTE WAMIMINIKA MAZOEZINI HADI ROONEY NA ZAHA

    IMEWEKWA JULAI 9, 2013 SAA 1:39 USIKU
    KOCHA David Moyes ameanza zama mpya Manchester United kwa kuingia uwanjani kuungana na wachezaji kuwafundisha katika Uwanja wa mazoezi wa klabu, Carrington leo.
    Kocha huyo mpya wa United aliungana na Msaidizi wake, Steve Round na alikuwa akifanya kazi yeye mwenyewe tofauti na kocha aliyemtangulia, Sir Alex Ferguson, ambaye alifurahia kuwaachia Mike Phelan na Rene Meulensteen kukochi timu.
    Mchezaji anayetaka kuondoka, Wayne Rooney, mchezaji mpya, Wilfried Zaha na kocha mchezaji, Ryan Giggs walikuwa miongoni mwa walioshiriki mazozi hayo ya leo.
    Welcome aboard: Manager David Moyes greets new signing Wilfried Zaha
    Karibu kijana: Kocha David Moyes akiwa na mchezaji mpya, Wilfried Zaha
    New boy: Zaha posted this picture on instagram
    Mwanzo mzuri: Zaha ameposti picha hii kwenye Instagram
    Zaha alilazimika kufanya vizuri ili kupambana na tetesi kwamba atatolewa kwa mkopo akakusanye uzoefu baada ya kusajiliwa kwa Pauni Milioni 15 kutoka Crystal Palace.
    Na winga huyo kinda wa umri wa miaka 20 kwa kuonyesha kufurahia kuanza kazi United, ameposti picha akiwa na jezi ya mazoezi ya timu hiyo akitweet: "Siku kubwa ya kwanza #MUFC,".
    Hands-on approach: David Moyes during a first team training session
    David Moyes akiongoza mazoezi mwenyewe leo
    On the ball: Moyes watches on
    Moyes akiwashuhudia wachezaji wake wakigongeana pasi mazoezini
    Box clever: Moye talks to assistant manager Steve Round
    Moye akizungumza na msaidizi wake, Steve Round
    Warm-up: Danny Welbeck and Rio Ferdinand
    Danny Welbeck na Rio Ferdinand
    All smiles: Wayne Rooney appeared to be making the most of fresh start (above) after falling out with Sir Alex Ferguson (below)
    Wayne Rooney alikuwepo leo, ingawa alimaliza vibaya msimu uliopita kwa kutofautiana na Sir Alex Ferguson (chini)
    Manchester United manager Sir Alex Ferguson (right) speaks with Wayne Rooney on the touchline
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MOYES AANZA ZAMA MPYA MAN UNITED...WACHEZAJI WOTE WAMIMINIKA MAZOEZINI HADI ROONEY NA ZAHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top