• HABARI MPYA

    Tuesday, July 16, 2013

    YANGA SASA WAMEKUWA, ASEMA HANS POPPE BAADA YA WAPINZANI KUSHUSHA KIFAA CHA NIGERIA

    Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JULAI 16, 2013 SAA 7:54 MCHANA
    MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wapinzani wao, Yanga SC sasa wanaanza kukua na kuachana na mambo ya kitoto, baada ya kuleta mshambuliaji kutoka Nigeria, Ogbu Brendan Chukwudi.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo, Poppe amesema kwamba kwa muda mrefu Yanga wamekuwa kama watu ambao hawajui soka kwa kusikilizia Simba SC inataka kumsajili nani na wao ndiyo wamfuate.
    Watani wanaanza kukua sasa; Zacharia Hans Poppe amewapongeza Yanga kwa hatua ya kutafuta wachezaji wao na si kusikilizia Simba SC wanataka kumsajili nani na wa wamfuate

    “Kwenye kikosi cha sasa cha Yanga kuna wachezaji wangapi wa Simba, wengi tu, yule Barthez (Ally Mustafa), Yondan (Kevin), Chuji (Athumani Iddi) na bado walitaka kuwasajili Amri Kiemba na Shomary Kapombe,”.
    “Usisahau Mbuyu Twite ni mchezaji ambaye tulikwishHamsajili sisi, wao wakacheza faulo na kumchukua juu kwa juu. Sasa namna hii hatuwezi kukuza soka na ushindani hata wa utani wetu wa jadi,”.
    “Lazima Yanga iwe na wachezaji wake na utaratibu pia wa kutafuta wachezaji wake, na sisi tuwe na wachezaji wetu na utaratibu pia wa kutafuta wachezaji wetu,”.
    “Ona kama sasa, sisi tumesajili mfungaji bora wa Kombe la Kagame, wao wameleta mfungaji bora wa Nigeria, sasa hawa watu wawili washindane kuzipatia matokeo mazuri timu hizi,”.
    Kifaa cha Jangwani; Ogbu Brendan Chukwudi akielekea Jangwani baada ya kuwasili jana usiku Dar es Salaam

    “Namna hii ndiyo mpira wa Tanzania utakuwa na si kusikia Simba kamfuata mchezaji na wewe unapeleka fedha zaidi kwa huyo huyo mchezaji, yale yalikuywa mambo ya kitoto na ya kishamba kabisa, ila sasa nawapongeza watani, wanaanza kukua,”alisema Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

    Kifaa cha Msimbazi: Hans Poppe 
    akiwa Amisi Tambwe baada 
    ya kumsainisha wiki iliyopita 

    Siku chache baada ya Simba SC kumpa Mkataba wa miaka miwili mfungaji bora wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Amisi Tambwe wa Vital’O ya Burundi, Yanga SC nayo imeleta mpachika mabao hatari wa Nigeria, Chukwudi kutoka Heartland, aliyetua nchini usiku wa jana.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: YANGA SASA WAMEKUWA, ASEMA HANS POPPE BAADA YA WAPINZANI KUSHUSHA KIFAA CHA NIGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top