Mazembe wakijifua Uwanja wa Marreikh jana, tayari kwa mchezo wa leo |
Mazembe wakiwasili uwanja wa Merreikh...
HATIMAYE hali imekuwa shwari kwa Tout
Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), baada ya jana
walipowasili mjini Khartoum kupokewa kwa kushambuliwa hadi basi lao kupasuliwa
vioo.
Mechi baina yao na wenyeji El Merreikh ya
Sudan, hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika inafanyika leo usiku.
Mazembe yenye washambuliaji wawili wa
Kitanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu jana usiku ilifanya
mazoezi kwenye Uwanja wa Merreikh.
Walitumia daika 22 ili kuuzoea Uwanja huo,
kuanzia saa 1:40 usiku kwa saa za huko. Uwanja ulikuwa umepambwa kwa rangi za
wapinzani wao, Merreikh nyekundu na njano.
Tayari kocha Lamine amekwishateua wachezaji
18 wa kushiriki mchezo huo, kati ya 22 aliokwenda nao.
Hao ni makipa: KIDIABA na MATAMPI - mabeki:
NKULUKUTA, KIMWAKI, Mihayo, HICHANI, KASUSULA, Sunzu, na NDONGA KASONGO - viungo:
Sinkala, Ochan, Ilongo, Kalaba, MPUTU, na LUSADISU Kasonde – wakati washambuliaji
ni Singuluma, SAMATA, LUNGU, Traore na KANDA.
Katika mchezo wa kwanza, Mazembe ilishinda
2-0 nyumbani, Samatta akifunga bao moja na leo inahitaji hata sare ili kusonga
mbele.
0 comments:
Post a Comment