WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya
Kombe Shirikisho, Simba wameendelea 'kuoga' manyanyaso na vitimbi vya kila aina
toka kwa wenyeji wao Al Ahly Shandy, ambapo juzi baadhi ya watu kwenye msafara
wa timu hiyo walilazimika kulala chumba cha mapokezi kufuatia kukosa vyumba kwenye
hosteli waliyofikia.
Gazeti la Mwananchi leo, limeandika kwamba
miongoni mwa walioadhibiwa na vitimbi hivyo ni pamoja na Mwenyekiti wa Simba,
Ismail Aden Rage na kocha Msaidizi wa makipa, James Kisaka ambao baada ya
kukosa vyumba walilazimika kulala kwenye makochi ya chumba cha mapokezi.
Viongozi wengine wa Simba, Mjumbe wa Kamati
ya Utendaji, Swedy Mkwabi na kiongozi wa msafara, Hussein Mwamba ambaye ni
mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, pia walikosa sehemu ya kulala na hivyo
wakalazimika kwenda kulala nje ya hosteli hiyo ya Shendi.
Mbali na kufanyiwa vitimbi hivyo, pia
Wekundu hao wa Msimbazi walilazwa kwenye hosteli badala ya hoteli hatua
iliyopelekea kugoma na kutishia kurudi mjini Khartoum licha ya umbali wa zaidi
ya kilomita 200 kwa gari kupitia barabara yenye jangwa kubwa na lisilo na makazi
ya watu.
"Hatuwezi kulala hapa, hii siyo hotel,
ni hosteli na kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) haikidhi
viwango", alilalama mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage.
Kwa mujibu wa kanuni ya CAF kifungu cha 7
(c), timu mwenyeji inatakiwa kuhakikisha kuwa timu mgeni inaishi katika hoteli
ya daraja la kwanza na pia msafara mzima unakaa katika hoteli moja.
Rage na viongozi wengine akiwemo mkuu wa
msafara ambaye ni mjumbe wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwamba
waliifanyia ukaguzi hosteli hiyo na kujiridhisha kuwa haikuwa na viwango.
Akizungumzia hali hiyo, mwakilishi wa timu
ya Shendi, Hamdy Ibn Hossein, alisema inatokana na ukweli kuwa mji wao ni mdogo
na hakuna hoteli nyingine kubwa kuliko hiyo mji mzima.
Hata hivyo, baada ya majadiliano kwa
pamoja, Simba iliamua timu ilale kwa hofu ya kuendelea kuwachosha wachezaji.
Hata hivyo, uongozi wa Simba unakusudia
kuwasilisha malalamiko rasmi kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutokana na
unyama inaofanyiwa nchini Sudan inakosubiri pambano lake dhidi ya Al Ahly
Shendi kesho.
Tangu iwasili nchini Sudan juzi, Simba
imekuwa ikifanyiwa vitendo visivyo vya kiungwana na wenyeji wake, Shirikisho la
Soka Sudan (SAF) na Al Ahly Shendi.
Jana, Simba ilifanyiwa vitendo hivyo kabla
ya kwenda katika mji wa Shendi itakakochezwa mechi hiyo na baada ya kufika
katika mji huo uliopo takribani kilomita 170 kutoka mji mkuu Khartoum.
Simba pia itapeleka malalamiko kutokana na
kuwekwa kwenye hosteli inayofanana na mabweni ya wanafunzi na imepewa vitanda
24 tu, huku msafara ukiwa na watu takribani 30.
Wakati ilipokuja Tanzania, Simba ililipia
gharama za watu 30 wa timu hiyo na kulikuwa na makubaliano kwamba na wao
watafanya hivyo wakati Wekundu watakapokwenda Sudan
|
Mike Tyson makes desperate marijuana plea to Donald Trump
-
A coalition of sport stars led by Tyson have penned a letter to the White
House amid a desperate plea to President Donald Trump.
11 minutes ago
0 comments:
Post a Comment