Tetesi za J'mosi magazeti Ulaya

DEMPSEY KAMALIZA MSIMU FULHAM

KIUNGO mshambuliaji, Clint Dempsey anaweza kuwa amecheza mechi yake ya mwisho katika klabu ya Fulham, baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, kutolewa kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachocheza mechi ya mwisho ya msimu huu kutokana na maumivu ya nyonga. Everton, Liverpool na Arsenal zipo tayari kumsajili.
MCHEZAJI wa Arsenal, anayecheza kwa mkopo Sunderland, Nicklas Bendtner mwenye umri wa miaka 24, anataka changamoto mpya nje ya klabu yake iliyomlea Arsenal.
KLABU ya Reading inajiandaa kumsajili mshambuliaji wa Tottenham, Jermain Defoe ahamishie cheche zake Uwanuja wa Madejski. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akisotea namba kwenye kikosi cha kwanza White Hart Lane msimu huu.
KOCHAn wa Everton, David Moyes anajiandaa kwa mazungumzo na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Bill Kenwright katika siku chache zijazo na ana matumaini ya kupewa fungu zuri la kufanyia usajili wa kusuka kikosi imara cha Uwanja wa Goodison Park, kitakachorejea Sita Bora katika Ligi Kuu.
KLABU ya Marseille ya Ufaransa, ina matumaini ya kumnyakua mshambuliaji wa Chelsea, Didier Drogba arejee kusini mwa Ufaransa akiwa ana umri wa miaka 34 na hiyo inatokakana na kushindikana kwa mpango wa kuongezewa mkataba wa miaka miwili Stamford Bridge.
KIUNGO wa kimataifa wa Japan, Shinji Kagawa atakuwa na mazungumzo ya mwisho na klabu yake, Borussia Dortmund, kuzungumzia mkataba mpya, kabla ya kuamua kuwakimbia mabingwa hao wa Ujerumani kwenda moja kati ya klabu za Ligi Kuu ya England, Manchester United, Arsenal na Tottenham zinazomuwania.
KLABU ya Lazio inajadili mpango wa kumsajili mshambuliaji 'aliyefulia' wa Manchester United, Dimitar Berbatov. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, amecheza tano tu za Ligi Kuu msimu huu.
KIPA wa Swansea, Michel Vorm mwenye umri wa miaka 29, amekataa ofa ya kuhamia Arsenal mwishoni mwa msimu, kwa sababu anataka kuendelea kucheza kila wiki.
HATIMA YA JT BADO KWA HODGSON
KOCHA wa England, Roy Hodgson bado hajaamua kumjumuisha kwenye kikosi chake, beki wa Chelsea, John Terry kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2012 licha ya taarifa za awali kwamba atamtema.