7 Mei, 2012 - Saa 12:22 GMT
Wasomali waanza kufurahia tena mechi za soka
Timu moja kusafiri hadi sehemu nyingine ni jambo linalowezekana sasa
Maeneo ya Somalia yameanza kucheza soka kutokana na uongozi wa Al-Shabaab kufifia
Manahodha wa timu zilizocheza mwishoni mwa wiki
MAENEO ya kati ya Somalia yameanza
kufurahia soka, huku uongozi wa Al-Shabaab ukiendelea kudidimia.
Wachezaji soka wa timu ya wilaya ya
Beled-weyne katika eneo la Hiiraan, waliweza kuifunga timu ya wilaya ya Guri-el
magoli 3-2 katika mechi ya kirafiki iliyochezewa Guri-el, eneo la Galgadud,
mwishoni mwa wiki.
Hii ilikuwa ni mara ya kwanza katika
kipindi cha miaka mitatu kwa vijana kutoka eneo la Hiiraan kuweza kusafiri na
kuingia eneo jirani la Galgaduud.
Eneo la Hiiraan limekuwa likisimamiwa na
kundi la Al-Shabaab ambalo limekuwa likisaidiwa na Al-Qaeda, na soka ilipigwa
marufuku katika eneo lote wakati kundi hilo likidhibiti sehemu hiyo.
Hayo yalikwisha wakati uongozi wa kundi hilo
la Kiislamu ulipokomeshwa mapema mwaka huu.
Mchezo huo wa kirafiki wa Guri-el
uliochezwa tarehe 5 ulisimamiwa na Ali Hassan Beile na vijana wengine waliokuwa
waamuzi, na waliopata mafunzo mwezi jana kutoka kwa chama cha soka cha Somalia.
Mwenyekiti wa kamati ya soka ya Galgadud,
Abdirashid Aden Roble, akiikaribisha timu kutoka eneo la Hiiraan, aliwaelezea
waandishi wa habari kwamba walifurahia sana kuwa wenyeji wa mechi hiyo ya miji
miwili kutoka kwa maeneo hayo mawili, ambayo wakaazi wake hawakuweza kuvuka
kutoka eneo moja hadi jingine kwa muda wa miaka mitatu, kutokana na makundi
tofauti ya Kiislamu kudhibiti maeneo yao.
Eneo la Hiiraan lilikuwa chini ya
Al-Shabaab, na eneo hilo lingine lilikuwa chini ya kundi ambalo linapinga
utumizi wa silaha la Ahlu sunna Wal Jama'a, na ambalo lina uhusiano mzuri na
serikali ya Somalia na pia jamii ya kimataifa.
"Ingawa timu yangu ya nyumbani ya
wilaya imeshindwa, ninafurahi sana kwamba tutaweza kuvuka mipaka ya wilaya na
kuendeleza mashindano ya soka, na shukrani zangu ni kwa shirkisho la soka
nchini Somalia, kwa kusaidia katika kuimarisha soka kati ya mataifa haya",
mwenyekiti Abdirashid Aden Roble alieleza.
Katibu mkuu wa shirikisho la soka la
Somalia, Abdi Qani Said Arab alizisifu wilaya zote mbili.
"Hili ndilo jambo ambalo shirikisho la
soka la Somalia limekuwa likitazamia, na tunatumaini maendeleo haya ya soka
yatachangia katika kuimarisha mashindano ya kabumbu katika maeneo mbalimbali
nchini", alielezea katibu mkuu wa SFF kupitia taarifa iliyotolewa
Jumatatu.
Alisema shirikisho la SFF mapema mwaka huu
lilikuwa limeanzisha mpango wa kuyasaidia maeneo ambayo yalitilia maanani
juhudi za kuimarisha soka.
Mafunzo yaliyofanyika katika jimbo la
Gal-Mudug mwezi uliopita yalikuwa na nia ya kuimarisha soka katika eneo hilo,
na baadhi ya vijana waamuzi waliopata mafunzo tayari wameanza kusimamia mechi
0 comments:
Post a Comment