• HABARI MPYA

    Thursday, May 17, 2012

    ARJEN ROBBEN AAHIDI KUCHEZA JUMAMOSI NA CHELSEA


    FC Bayern München, Arjen Robben
    Arjen Robben
    KIFAA cha Bayern MunichArjen Robben amewaahidi mashabiki atakuwa tayari kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Chelsea Jumamosi.
    Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Uholanzi amekuwa akitiliwa shaka kucheza mechi hiyo, baada ya kukosa sehemu mbili zilizopita za mazoezi ya klabu hiyo kutokana na baridi kali.
    "Niliathiriwa na baridi kali," Robben alisema akihojiwa na Sport-Informations-Dienst. "Ilibidi niwe makini ili nisipoteze nguvu zangu.kama nisingekuwa na homa ya kiwango cha nyuzi 40 au 41, ningekuwa uwanjani."
    Mapema Alhamisi ya leo, Robben alisema kwamba Bayern ina uwezo wa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa, ambalo haijalitwaa tangu mwaka 2001.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARJEN ROBBEN AAHIDI KUCHEZA JUMAMOSI NA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top