• HABARI MPYA

    Friday, May 04, 2012

    ARSENAL FULL SKWADI WAJA AFRIKA AGOSTI


    LABU ya Arsenal inatarajiwa kusafiri na kikosi chake cha kwanza hadi Nigeria mwanzoni mwa msimu ujao, kucheza mechi za kirafiki zxa kujiandaa na msimu mpya mjini Abuja Jumapili  ya Agosti 5.

    Hiyo itakuwa mara ya kwanza Washika Bunduki wa London kucheza katika ardhi ya Nigeria, timu ya Arsene Wenger itacheza kwenye Uwanja wa kuchukua mashabiki 60,000,  Abuja National Stadium.

    Mara ya mwisho klabu hiyo kuzuru Afrika ilikuwa ni katika ziara ya Afrika Kusini Julai mwaka 1993.

    Kabla ya ziara ya Nigeria, Arsenal itaanzia China na Malaysia mwezi Julai, kufuatia mafanikio ya ziara mwaka jana bara la Asia.

    Ikiwa Asia, Arsenal itacheza mechi nne mjini Kuala Lumpur, dhidi ya kombaini ya Malaysia Jumanne ya Julai 24 kabla ya kwenda China, kucheza na Manchester City mjini Beijing Ijumaa ya Julai 27, ikifuiatiwa na safari ya Hong Kong for watakapocheza na Kitchee FC Jumapili ya Julai 29.

    Taarifa zaidi kuhusu ziara ya Nigeria zitapatikana baadaye hapa hapa BIN ZUBEIRY kutoka Arsenal.com mara tu zitakaposhuka.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL FULL SKWADI WAJA AFRIKA AGOSTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top