Friday's gossip column
TRANSFER GOSSIP
BEKI wa pembeni wa Barcelona, Dani Alves, mwenye umri wa miaka 28, anajipanga kuipiga chini ofa ya klabu ya Manchester City na kubaki na vigogo hao wa Catalan.
KLABU ya Manchester United inaaminika ipo karibu mno kukamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Japan, anayechezea Borussia Dortmund, Shinji Kagawa, na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu Old Trafford.
KLABU ya Manchester City inamtaka nyota wa Tottenham, Gareth Bale mwenye umri wa miaka 22, kwa dau la pauni Milioni 40 taslimu pamoja na kumtoa mchezaji mmoja.
KLABU ya Arsenal inakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Tottenham Hotspur katika kuwania saini ya mchezaji Junior Hoilett sambamba na Jan Vertonghen na Eden Hazard
KLABU za Newcastle na Reading zipo kwenye ushindani mkali wa kuwania saini ya mchezaji wa Barnsley mwenye thamani ya dau la pauni Milioni 2, kiungo mbichi mwenye umri wa miaka 21, Jacob Butterfield.
WINGA wa klabu ya FC Twente mwenye umri wa miaka 19, Ola John, anatakiwa na klabu za Sunderland na Aston Villa, ingawa mwenyewe anafikiriwa kukubali ofa ya Benfica, ambao wanataka kununua huduma yake kwa dau la pauni Milioni 9, kwa mujibu wa gazeti la Ureno la A Bola.
KLABU ya Liverpool inamuwania mchezaji wa Manchester City, Mholanzi Nigel de Jong.
KLABU ya Arsenal inatumai kuendelea kuishi na Mchezaji Bora wa Mwaka England, Robin van Persie na imesukumwa kufanya hivyo kutokana na Manchester City kumtaka mshambuliaji huyo kwa dau la pauni Milioni 20.
OTHER GOSSIP
KOCHA Fabio Capello amemuonya Roy Hodgson kwamba atakutana na wakati mgumu wa kutengeneza timu imara ya ushindi katika kikosi cha timu ya taifa ya England, kabla ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya zitakazofanyika Poland na Ukraine majira ya joto mwaka huu.
Habari kamili: The Times (Subscription required)
KOCHA Jose Mourinho amemuambia Roman Abramovich atabaki Real Madrid na hatarejea Stamford Bridge tena.
KIUNGO wa Tottenham, Rafael van der Vaart amemwagia sifa Harry Redknapp kwamba ni kocha maalum, "special manager" na anatumai kubaki katika klabu hiyo yenye maskani yake, White Hart Lane..
AND FINALLY
KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Cristiano Ronaldo alifanya kitu kisicho cha kiungwana akishangilia bao lake baada ya Real Madrid kuifunga Athletic Bilbao na kutwaa ubingwa wa Hispania, akimkejeli Javi Martinez, nyota wa Bilbao na mwanasoka wa kimataifa wa Hispania, ambaye alitolewa kwa kadi nyekundu kwenye mechi hiyo.
0 comments:
Post a Comment