KWA sasa kuna watu ambao wako msituni, wanatumia baadhi ya
wanachama wa Yanga na Waandishi wa Habari kuleta vurugu katika klabu ya Yanga,
lengo lao kuuangusha uongozi uliopo madarakani.
Watu hao wanajulikana na silaha yao ni fedha- inawapa jeuri
ya kutaka kuivuruga Yanga.
Hadi kufikia hapa, Yanga inakosa hata nafasi ya pili katika
Ligi Kuu, wao wamechangia kwa kiasi kikubwa. Kujiuzulu kwa Seif Ahmad ‘Magari’
na Abdallah Bin Kleb katika Kamati ya Utendaji, inasemekana pia kumetokana na
ushawishi wao.
Nasikitika watu hawa ni wageni sana Yanga na hawaijui
historia ya klabu hiyo. Wana Yanga ni wazito kuamua, kwa sababu wana subira,
ila yakiwafika kooni huwa ni wati tofauti sana.
Huwa hawaangalii sura wala hadhi ya mtu.
Mungu amrehemu, Abbas Gulamali, alimwaga fedha nyingi Yanga
na akakarabati hadi jengo, kwa ujumla alifanya makubwa nay a kihistoria- lakini
alipotofautiana kimisimamo na wenye Yanga yao, yalimgeukia.
Reginald Mengi alikuwa ana heshima kubwa Yanga na akajitolea
kusuluhisha mgogoro wa Yanga Asili na Yanga Kampuni.
Awali, walimsikiliza na kwenda naye sawa, lakini alipotofautiana
na wenye Yanga yao, yalimgeukia pale Star Light Cinema na hadi leo hajakanyaga
tena kwenye shughuli ya Yanga.
Nani asiyejua Mengi ni Yanga mzuri na milionea ambaye leo
hii akiangukiwa klabu itakuwa baab kubwa? Tunakubali udhaifu wa uongozi ndani
ya klabu, lakini suluhisho lake si kuleta vurugu klabuni.
Kama watu wana vita binafsi, wapambane wao kwa wao bila
kuiumiza Yanga. Lloyd Nchunga ni mwana Yanga mmoja tu kati ya mamilioni. Haiwezekani
mtu apambane na Mwenyekiti wa Yanga kwa kuinyima Yanga ubingwa- hata nafasi ya
pili na bado anataka timu ifungwe na Simba. Huyu si mwana Yanga- ni mnafiki. Ni
mbinafsi- na maana yake anataka hata kuwapo Yanga kwa maslahi yake binfasi.
Yanga wa kisasa wanataka umoja, mshikamano na mafanikio ya
uwanjani. Yanga wa kupewa noti nyekundu walete malumbano na migogoro isiyo na
tija klabuni, hao ni wa kuwaangalia mara
mbili.
Wewe una umgovi na Nchunga au Yanga, hebu jiulize? Kwa nini
uwanyime raha wana Yanga mamilioni kwa mamilioni kwa fedha zako?
0 comments:
Post a Comment