![]() |
| Tegete akiwa na kocha Papic kushoto, hii ilikuwa Mwanza mwaka juzi alipofunga bao pekee lililoilaza Simba. |
WACHEZAJI wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam
wamewasuta wazee na wanachama wa klabu hiyo, wanaodai kwamba wao wanaidai klabu
zaidi ya Sh Milioni 270.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY asubuhi hii kwa
niaba ya wachezaji wenzake, mshambuliaji wa Yanga, Jerson Tegete alisema
wachezaji waliingia kwenye mechi dhidi ya Simba Jumapili wakiwa hawadai chochote
kwa uongozi.
Jana, Katibu wa Baraza la Wazee la klabu, Ibrahim
Ally Akilimali alisema kipigo cha 5-0 kimetokana na wachezaji kutokuwa na morali
kwa sababu wanaidai fedha nyingi klabu.
“Hakuna anayedai, wote tulilipwa madai yetu
kabla ya mechi, tena yote,”alisema Tegete.
Kwa sasa Yanga kuna mgogoro unaosababishwa
na wazee wa klabu hiyo, ambao wanampiga vita Mwenyekiti wa klabu hiyo, Wakili Lloyd
Baharagu Nchunga wakitaka aondoke madarakani.
Inadaiwa wazee hao wanatumiwa na kiongozi
mmoja wa zamani wa Yanga, ambaye nia yake awe yeye bosi wa klabu.
Inadaiwa hata kipigo cha 5-0, kilitokana na
wapinzani hao wa Nchunga kuwahonga baadhi ya wachezaji wacheze chini ya
kiwango.
Na kauli yao ya kusema wachezaji hawana
morali ndio maana walifungwa, ilifuatia Nchunga kusema kuna wachezaji
walihujumu timu na watafukuzwa.
Walichokifanya wazee hao, walikuwa kama
wanawatetea wachezaji wasifukuzwe- wakati kihistoria klabu ilikwishawahi
kufukuza wachezaji baada ya kufungwa 4-1 na Simba mwaka 1994.



.png)
0 comments:
Post a Comment