DROO ya pili ya Promosheni inayoendelea ya kampuni ya bia ya
Serengeti inayojulikana kama‘Vumbua hazina chini ya kizibo’ imefanyika leo
katika ofisi za kampuni hiyo maeneo ya Oysterbay jijini Dar Es salaam.
Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni
ya bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda amesema leo asubuhi katika mkutano na
waandishi wa habari ofisini kwake, Oysterbay, Dar es Salaam kwamba kupitia
bidhaa zao, Serengeti Premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha
promosheni nchi nzima ijulikanayo kama “ VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO.’
Teddy ‘Smart Lady’ alisema Promosheni hii
ya aina yake iliyosheheni zawadi mbalimbali kubwa na ndogo kama vile Jenereta
(kangavuke), Pikipiki, Bajaji, Gari ndogo aina (saloon) na zawadi zingine
nyingi zikiwemo pesa taslimu. Katika promosheni hii zawadi za thamani zaidi ya
Tsh MILLIONI 780 kushindaniwa.
“Droo hiyo ilihudhuriwa na waandishi wa
habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na
nje ya kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH
MOBILE, wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers ili
kuhakikisha washindi wote wanapatikana kihalali,”alisema.
“Tayari tuna washindi zaidi ya elfu moja
mia tano, wamejishindia pesa taslimu na kuzipata kupitia njia ya MPESA. Hawa washindi ni pamoja na wanaoshinda bidhaa
zenyewe zilizoorodheshwa katika promosheni hii.
Vile vile, kama mlivyoshuhudia
asubuhi ya leo, tumepata washindi wawili wa jenerata, na sio mmoja kama ilivyo
kawaida . Hii ni kwa sababu katika
promosheni hii, kuna vigezo na masharti yanayozingatiwa” aliongeza.
Alisema masharti ya promosheni hii wanayazingatia,
kwa sababu hiyo, mshindi wa wiki iliyopita wa jenerata ilikuja kugundulika
hakustahili kushiriki katika promosheni hii.
“Tunataka kuwaeleza watanzania kwamba hii promosheni ni ya uhakika na kwa
kweli mnavyoona, ina uangalizi mkubwa na inaendeshwa kwa umakini kabisa. Nawaomba wateja wetu waendelee kushiriki ili
waendelee kushinda.” Aliongeza mkurugenzi huyo.
Washindi
katika droo ya leo waliojishindia jenereta ni Amadeus Minja mkazi wa
pugu na Agnes Msengi wote wakia ni wakazi wa jijini Dar Es Salaam na Ibrahim
Kimambo mkazi wa Tabata Kimanga jijini Dar Es Salaam aliyejishindia Pikipiki
. Allan Peter Chonjo, Meneja wa Bia ya
Serengeti Premium Lager alipiga simu kwa washindi na ilikuwa dhahiri kwamba
washindi walishtuka na kufurahia ushindi wao.
Baada ya maongezi machache yaliyofanyika kwa njia ya simu washindi hao
waliweza kujieleza vizuri majina yao kamili na wanapopatikana ili waweze kupatikana
siku chache zijazo kwenye hafla fupi ya kuwakabidhi zawadi zao.
MAELEKEZO:
Nunua bia ya Serengeti Premium Lager,
Tusker Lager au Pilsner Lager fungua kisha angalia ndani ya kizibo utapata namba saba zilizochanganyika na
herufi.
Fungua sehemu ya kutuma ujumbe mfupi kwenye
simu yako, nakili namba na herufi hizo mfano TS5555P, na uzitume kwenda 15317
na utapokea ujumbe mfupi wa maneno ambao utasema kama umejishindia pesa taslimu
kati ya shilingi 10,000 au 50,000 au 100,000 ambayo itatumwa kwako kwa njia ya
MPESA. Au unaweza kupata ujumbe utakao kwambia kuwa namba yako imeingia kwenye
droo ya bahati nasibu na utaweza kujishindia zawadi kubwa kama vile jenereta,
gari ndogo , bajaji au pikipiki
Katika promosheni hii pia unaweza kujipatia
bia ya bure papo hapo kila utakapoona alama ya chupa ndani ya kizibo na unaweza
kupata kati ya bia tatu zilizoainishwa katika promosheni hii. Pia unaweza kupata maelekezo katika
vipeperushi na magazeti.



.png)
0 comments:
Post a Comment