![]() |
| Wa wa Taifa Queens michuano ya Afrika ya Netoboli, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. |
Taifa Queens tangu mwanzo walionekana
kupania kufanya vizuri katika mchezo huo ambao mgeni rasmi alikuwa mke wa Rais
Mama Salma Kikwete.
Hadi robo ya kwanza inamalizika, Taifa
Queens walikuwa mbele kwa mabao 13-3 na kuendelea
kuwachachafya wapinzani wao na kumaliza
robo ya tatu wakiendelea kuongoza kwa 40-13.
Wakicheza kwa uelewano mkubwa, Taifa Queens
iliyopiga kambi kwa takribani miezi mitatu katika Shule ya Sekondari ya Filbert
Bayi Kibaha, ilizidi kuwapeleka puta wapinzani wao ambao hawakufunga hata bao
moja katika robo ya mwisho.
Akizungumza wakati wa ufunguaji wa
mashindano hayo, Mama Salma Kikwete alisema mashindano hayo yasaidie kukuza
ushirikiano miongoni mwa nchi za Afrika.
Alitoa wito kwa viongozi wa michezo na
taasisi za mahusiano ya kimataifa katika nchi za Kiafrika kutumia vizuri fursa
za michezo katika kukuza na kuboresha mahusiano ya nchi za Afrika.
Naye Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Dk. Fenella Mukangara alivitaka vyama vya michezo kujipanga vizuri ili
kuhakikisha vinafanikisha malengo yao .
Mashindano hayo yanayoshirikisha nchi saba
yanaendelea tena leo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na hakuna kiingilio.


i.jpg)







.png)
0 comments:
Post a Comment