![]() |
| Wachezaji wa Simba wakishangilia ubingwa wao |
KIKOSI cha Simba kinagtarajiwa kuondoka leo
mchana kwenda Sudan kupitia Nairobi, Kenya tayari kwa mchezo wa marudiano wa
Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly Shandy baada ya kukwama kuondoka kutokana
na majambazi kuvunja na kuiba katika ubalozi wa Sudan.
Juzi usiku majambazi walivunja sefu ya
kuhifadhia fedha na kuiba zaidi ya dola 40,000 ubalozini hapo pamoja fedha
nyingine pamoja na kuiba kompyuta zote zinazotumika kuhifadhia kumbukumbu
mbalimbali.
Kutokana na hali hiyo, Simba walikwama
kupata viza zao juzi na jana na zinataraji kutolewa leo asubuhi kabla ya
kuondoka saa 10:00 kwenda Sudan kupitia Nairobi ikiwa na wachezaji wote wa timu
hiyo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Faustine
Shilogile alithibitisha juzi kutokea tukio hilo.



.png)
0 comments:
Post a Comment