![]() |
| Okwi |
WAKATI wawakilishi wa Tanzania kwenye
michuano ya Kombe la Shirikisho, Simba wakiondoka leo kwenda Khartoum, Sudan
tayari kwa mchezo wa marudiono dhidi ya Al Ahly Shendi, washambuliaji nyota wa Wekundu hao wa
Msimbazi, Emmanuel Okwi na Felix Sunzu wameingia kwenye rekodi ya wafungaji
bora Afrika katika michuano ya Kombe la Shirikisho la soka Afrika.
Gazeti la Mwananchi leo, limeandika kwamba Okwi,
raia wa Uganda na Felix Sunzu ambaye ni Mzambia, wote wametajwa kuwa na mabao
matatu kila mmoja kwa mujibu wa mtandao wa tensport.com.
Mshambuliaji huyo anayechezea pia Uganda
Cranes, alifunga bao moja dhidi ya Entente Sportive de Setif katika mchezo wa
kwanza kati ya mawili walioshinda mabao 2-0 Dar es Salaam na moja likifungwa na
Haruna Moshi.
Mchezo wa marudiano, Okwi alifunga moja
wakati Simba ikilala mabao 3-1. Mshambuliaji huyo alifunga dhidi ya Al Ahly
Shendi kati ya mabao matatu huku mengine yakifungwa na Boban na Patrick
Mafisango.
Kwa hali hiyo, Boban na Sunzu kila mmoja
wana mabao matatu. Sunzu aliyafunga katika mchezo walioshinda mabao 2-1 dhidi
ya Kiyovu ya Rwanda na lingine likifungwa na Parick Mafisango.
Mbali na wachezaji hao, wengine wenye mabao
matatu ni Komara, Niamba wote wa Leopards ya Congo, Chinyengetere (Hwange ya
Zimbabwe, Moco (InterClube (Angola) na Raouf (ENPPI, Misri) na Seri wa Asec
Mimosa ya Ivory Coast.
Mpaka sasa Fiston (Lydia Academic, Burundi)
na Girma wa St George ya Ethiopia wana mabao manne kila mmoja.



.png)
0 comments:
Post a Comment