![]() |
| Wachezaji wa Man City wakipongezana katika moja ya mechi za Ligi Kuu walizoshinda msimu huu |
BILIONEA na mmiliki wa klabu ya Manchester
City, Sheikh Mansour amewaahidi wachezaji wake posho nene ya Sh600 milioni
(sawa na pauni 250,000) kila mchezaji iwapo watafanikiwa kuipiku Manchester
United na kutwaa ubingwa.
Kikosi cha Kocha Roberto Mancini kiko
jirani zaidi na kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa wa England kwa mara ya kwanza
tangu ilipofanya hivyo mara ya mwisho mwaka 1968.Tajiri Mansour anaamini zawadi
ya ubingwa wa England haitoshi kuwafurahisha wachezaji wake, kwa maana hiyo
amekubali kuzama mfukoni mwake na kutoa ziada ili kuwapa wachezaji wake.
Kwa mujibu wa gazeti la 'The Daily Star',
bosi Mansour amewaambia wachezaji wake kama wanataka pesa, basi wahakikishe
wanatwaa ubingwa msimu huu.
Man City inamaliza msimu wa ligi kwa
kuvaanana timu ya Queens Park Rangers kwenye Uwanja wa Etihad Jumapili
inayofuata, na ili iweze kuweka rekodi hiyo mpya italazimika kuifunga QPR
inayohitaji pointi ili ibaki Ligi Kuu msimu ujao.
Taarifa zaidi zinadai kuwa bilionea huyo
yuko tayari kumwaga kiasi cha pauni 4.5milioni (Sh11.3 bilioni) kama motisha
kwa timu nzima.
Manchester United inahitaji miujiza kutetea
taji msimu huu pamoja na kwamba wanalingana kwa pointi na City, lakini
wapinzani wao wana utajiri wa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.Ni
ushindi tu utakaowapa rekodi mpya ya kutwaa ubingwa wa England walioutafuta kwa
zaidi ya miaka 42. United wanamaliza ligi kwa kuvaana na Sunderland.
Wakati City wakiandaliwa bonas hiyo iwapo
watatwaa ubingwa, timu ya Blackburn imeshuka rasmi daraja baada ya usiku wa
kuamkia jana kufungwa bao 1-0 kwenye uwanja wa nyumbani dhidi ya Wigan.
Blackburn ilikuwa ikihitaji ushindi ili
ijinusuru na anguko hilo, lakini walijikuta wakipoteza mchezo huo mbele ya
mashabiki wao dhidi ya timu ambayo tayari ina uhakika wa kucheza ligi msimu
ujao.
Bao lililoizamisha Rovers lilifungwa kwa
kichwa na Antolin Alcaraz aliyemaliza mpira wa kona uliochongwa na Latics ndani
ya dimba la Ewood Park.



.png)
0 comments:
Post a Comment