4 Mei, 2012 - Saa 14:06 GMT
Chelsea ina mipango ya kutobomoa mabomba ya kutolea moshi ikiwa itajenga uwanja mpya katika kituo cha Battersea
KLABU ya Chelsea imewasilisha ombi la kutaka
kukinunua kituo cha kuzalisha umeme cha Battersea mjini London, na klabu kina
mipango ya kujenga Uwanja mpya wa soka mahali hapo, utakaoweza kuwapokea
mashabiki 60,000.
Mabomba manne ya kutolea moshi katika
uwanja huo yatabaki, na kuwa ni sehemu moja ya upande wa kusini mwa uwanja
itakayokuwa na viti 15,000.
Chelsea imeelezea imekuwa vigumu kupanua
uwanja wao wa Stamford Bridge, na kiuchumi, mpango huo haufai, na vile vile
klabu kimekuwa na matatizo katika kuwashawishi wahusika kuidhinisha mipango
yake ya upanuzi.
Klabu kimeongezea kwamba kuna wengine
wanaotaka kukinunua kituo hicho.
"Hakuna uhakika kwamba ombi letu
litafaulu," taarifa ya klabu imeelezea.
"Lazima pia kusisitiza kwamba kwa
kuwasilisha ombi la kukitaka kituo cha Battersea cha kuzalisha umeme, hayo
hayamaanishi moja kwa moja uamuzi kamili wa kuuhama uwanja wa Stamford
Bridge."
Klabu kimeelezea kwamba kitazingatia
masharti ya kutobomoa ukumbi uliopo katika eneo hilo na pia chumba cha
kuendesha mitambo ya umeme, kwa kuzingatia sheria zinazohusiana na kuhifadhi
majumba ya kale.
Kufanya hivyo itakuwa ni nafasi ya kujenga
uwanja wa kupendeza wa kisasa, lakini pia kwa kuhifadhi na kuimarisha mandhari
ya eneo hilo.
Klabu pia kina mipango ya kujenga maduka,
nyumba na afisi katika eneo hilo, na vile vile kuimarisha usafiri kupitia treni
za chini kwa chini
Uwanja wa Stamford Bridge, unaoweza
kuruhusu mashabiki 42,000, hauwezi kulinganishwa na uwanja wa kisasa kabisa wa
Imarati wa Arsenal, ambao unaweza kuingiza mashabiki 60,000, huku ule wa
Manchester United wa Old Trafford ukiwa na uwezo wa kuwaruhusu mashabiki
76,000.
0 comments:
Post a Comment