Panoramic
KLABU ya Manchester City imetangaza mpango wa kuingia mkataba wa miaka mitano na Nike kuanzia msimu wa 2013-14.
The Blues hao wataendelea kudhaminiwa na Umbro msimu ujao kwa vifaa vyote vya michezo, kuanzia vya mazoezi na bidhaa zinazohusiana na klabu hiyo zitaanza kutengenezwa na kampuni ya michezo Marekani.
Mkataba huo, unamaanisha City watachangia mdhamini na wapinzani wao wa Jiji la manchester, Manchester United, ambao wamekuwa wakidhaminiwa na Nike
tangu mwaka 2002.
Rais wa Nike, Charlie Denson ameaimbia tovuti ya klabu hiyo kwamba; “Tumevutiwa na na nafasi hii ya kuendeleza uhusiano wetu baina ya City na Nike Inc, ambayo tayari imejenga uhusiano wa ushirikiano na klabu hiyo kwa kupitia Umbro.”
Mkataba mpya wa udhamini utawezesha kupatikana fedha nyingi za kusajilia wachezaji wapya kwenye timu hiyo ambayo tayari inapigwa zengwe kwa kumwaga fedha nyingi katika usajili.
John MacBeath, Ofisa Mtendaji Mkuu wa City alisema: “Tunatazamia kuimarisha zaidi ushusiano wetu na familia ya Nike,"alisema.
0 comments:
Post a Comment