HAPA bongo Simba walikuwa wana striker mmoja alikuwa anaitwa Adam Sabu (sasa marehemu)- ambaye kutokana na kufunga kwake mabao, aliitwa Gerd Muller.
Huyu ni mshambuliaji hatari wa zamani wa Ujerumani, ambaye katika kitabu chake kiitwacho Brilliant
Orange: The Neurotic Genius of Dutch Football, David Winner anaandika; Muller
alikuwa mfupi, hana sura ya mvuto na hana kasi; hakuwa mchezaji unayeweza kusema ni mkali, lakini alikuwa
mzuri katika mipira ya juu na uchu wa kufunga mabao. Miguu yake mifupi
ilimwezesha kugeuka haraka na kukimbia kiasi cha kufanya wachezaji wa timu
pinzani kuanguka wanapomkimbiza. Aidha alikuwa na uwezo wa kufunga katika
mazingira magumu.
Huyo ni Gerhard ‘Gerd’ Müller aliyezaliwa
Novemba 3, mwaka 1945 mjini Nordlingen, ambaye
alikuwa mchezaji muhimu na mfungaji bora wa zamani nchini Ujerumani.
Ufungaji bora wa Müller unajidhihirisha
yenyewe. Amefunga magoli 68 katika michezo 62 akiwa na timu ya taifa, mabao 365
katika michezo 427 ya Bundesliga (Ligi Kuu nchini Ujerumani) na rekodi ya mabao
66 ya kimataifa katika michezo 74 ya Klabu Ulaya. Müller kwasasa anashikilia
nafasi ya nane kwa ufungaji bora katika mechi za kimataifa licha ya kucheza
michezo michache ukilinganisha na wachezaji wengine katika orodha ya wachezaji
15 bora. Majina yake ya utani ni “Bomber der Nation” (Mlipuaji mzuri kuongoza
taifa) na “kleines dickes Müller” (Mfupi mnene Müller, uongo wa mkubwa).
Mwaka wa 1970, Müller alichaguliwa Mchezaji
Bora wa Mwaka Ulaya baada ya mafanikio msimu huo akiwa na Bayern Munich ambapo
alifunga mabao 10 katika Kombe la Dunia 1970 FIFA. Kabla ya bao ambalo alifunga
Ronaldo katika mechi dhidi ya Ghana hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia 2006,
Müller alikuwa anashikilia ufungaji bora wa mashindano hayo kwa mabao 14,
rekodi iliyodumu kwa miaka 32.
Alianza kucheza soka katika klabu ya TSV
1861 Nördlingen. Müller alijiunga na FC Bayern Munich mwaka 1964 ambapo
aliungana na wachezaji nyota wa baadaye Franz Beckenbauer na Sepp Maier. Klabu
hii (Bayern Munich) aliyokuwa anaichezea Müller ilikuja ikawa maarufu. Akiwa na
Bayern Munich, Müller alishinda mataji mengi katika miaka ya 1960 na 1970:
Alishinda Ubingwa wa Ujerumani mara nne, Ubingwa wa Ulaya mara tatu, Ubingwa wa
Mabara mara moja, na Ubingwa wa Mabingwa Ulaya mara moja. Uimara wake wa
kufunga mabao ulimfanya awe mfungaji bora nchini Ujerumani mara saba na
mfungaji bora Ulaya mara mbili. Müller anashikilia ufungaji bora ndani ya msimu
moja katika Bundesliga kwa rekodi ya mabao 40 katika msimu wa 1971–72.
Muller alifunga mabao 68 katika michezo 62
akiwa na timu ya Ujerumani Magharibi. Alianza kuichezea timu ya taifa mwaka wa
1966 na kustaafu Julai 7, 1974 baada ya kushinda Kombe la Dunia lililoandaliwa
katika uwanja wake wa nyumbani jijini Munich. Alifunga bao la ushindi katika
mechi la fainali ambapo waliwafunga Uholanzi 2-1. Mabao yake manne na yale 10
katika Kombe la Dunia 1970 lilimfanya awe mfungaji bora katika michuano hiyo na
jumla ya mabao 14; rekodi ambayo ilidumu hadi mwaka 2006 ambapo Ronaldo
alimpiku. Cha kushangaza ni kwamba Kombe la Dunia 2006 ilifanyika nchini
Ujerumani. Ronaldo, mshambuliaji wa Brazil, alifunga bao la 15 na kumpiku
Müller katika mechi dhidi ya Ghana iliyochezwa Juni 27, 2006.
Baada ya kucheza Bundesliga, alienda Marekani
ambapo alijiunga na Fort Lauderdale Strikers mwaka ya 1979 inayoshiriki Ligi ya
Marekani Kaskazini. Alicheza misimu mitatu na timu hii akifunga mabao 38 na
nyakati moja kufika fainali lakini kupoteza mwaka 1980.
Baada ya Müller kustaafu soka mwaka 1982,
alijikuta akiwa mlevi wa kupindukia. Hata hivyo, wafariki zake katika timu ya
Bayern Munich walimsihi kwenda kupata ushauri nasaha. Na alipopata nafahu,
alipewa kazi ya ukocha katika timu ya Bayern Munich II ambapo anafanya kazi
hadi leo. Pia kuna vifaa vya michezo vinavyotolewa na kampuni ya Adidas chini
ya jina la Gerd Müller. Ni sehemu ya mzigo mpya ya adidas. Julai mwaka 2008,
uwanja wa Rieser Sportpark uliopo in Nördlingen ambapo Müller alianza kucheza
soka ulibadilishwa jina na kuitwa Gerd-Müller-Stadion kwa heshima ya
mshambuliaji huyo.
WASIFU WAKE:
JINA: Gerhard Müller
KUZALIWA: 3 Novemba 1945 (Miaka 65)
ALIPOZALIWA: Nordlingen, Ujerumani
KLABU ALIZOCHEZEA:
Mwaka Klabu
1963–1964 1861
Nördlingen (Mechi 32, mabao 51)
1964–1979 Bayern
Munich (Mechi 453, mabao 398)
1979–1981 Fort
Lauderdale Strikers (Mechi 80, mabao 40)
(Tangu 1966 hadi 1974, aliichezea Ujerumani
Magharibi mechi 62, akaifungia mabao 68)
0 comments:
Post a Comment