WAZEE wa klabu ya Yanga, wakiongozwa na ‘kinara
wa migogoro’ klabuni, Mzee Ibrahim Akilimali, ambaye rekodi zinaonyesha
hakubaliki Yanga, kwa sasa wanampiga zengwe Mwenyekiti wa klabu hiyo, Wakili
Lloyd Baharagu Nchunga.
Mzee Akilimali historia inaonyesha
hakubaliki Yanga, kwa sababu mwaka 1993 alitaka kugombea Uenyekiti, lakini
alipofika kwenye ukumbi wa mkutano, Uwanja wa Ndani wa Taifa, alipoona joto la
uchaguzi huo kwamba hakubaliki alitaka kujitoa ili awanie Umakamu Mwenyekiti na
huko pia wakamzuia kugombea.
Wazee hawa ambao wanatamba kwenye vyombo
vya habari wakimpiga vita Nchunga, historia inaonyesha wamekuwa bughudha kwa
uongozi wa klabu, si wakati huu tu wa Nchunga, bali hawa ndio waliompindua mzee
mwenzao, marehemu Rashid Ngozoma Matunda (Mwenyezimungu amrehemu), kabla
hawajagonga mwamba kwa jemedari, Wakili Imani Omar Madega, ambaye aliwapsha na
wakarudi nyuma na kumuacha aongoze klabu, hadi muda wake ulipofika akaachia
madaraka kwa amani, tena akishangiliwa na wana Yanga PTA.
Madega aliwashushia kauli nzito, akisema; “Wazee
na wanachama wachache waroho wa Yanga, kuweni macho na msiwasaliti wazee
wenzenu, ambao walifanya juhudi kuifanya Yanga iwe na jina kubwa, mkiendelea
kufanya hivyo kwa hakika historia itawahukumu, uongozi uko imara kutetea
maslahi ya Yanga,”.
Madega aliwapa dongo hili, wakati wazee hao
walipokuwa wakidaiwa kutumiwa na tajiri mmoja ili kumpindua Madega, kwa sababu
hakuwa tayari kufuata matakwa ya tajiri huyo.
Kauli hii, Madega aliitoa Oktoba 11, mwaka
2007 mjini Dar es Salaam.
Sasa, Wazee hawa tena, wanampiga zengwe
Nchunga, je kwao nani atafaa kuongoza Yanga? Tujadili.



.png)
0 comments:
Post a Comment