| Dembele |
KLABU za Manchester United, Manchester City
na Chelsea zimeungana katika mbio za kuwania saini ya kiungo na mshambuliaji
Moussa Dembele wa Fulham, BIN ZUBEIRY ameipata hiyo.
Mpachika mabao huyo amekuwa akifuatiliwa na
klabu zote kubwa za Ligi Kuu England, ili kupata saini yake.
BIN ZUBEIRY imepata habari kutoka Goal.com kwamba
Machi, mwaka huu Arsenal, Liverpool na Tottenham zilikuwa zinamfuatilia kwa
karibu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24.
Na mwansoka huyo wa kimataifa wa Ubelgiji,
ametoa mchango mkubwa kwa Fulham hadi inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa
Ligi Kuu msimu huu, jambo ambalo limezifanya klabu kubwa zimsake kwa ofa ya
mshahara mnono.
Thamani ya Dembele inakadiriwa kuwa kati ya
pauni Milioni 12 hadi 15 ambazo Fulham, inaweza kupokea kumuuza.
Pamoja na hayo, Dembele ana mwaka mmoja tu
zaidi katika mkataba wake wa sasa na Fulham na hata kumuuza kwa dau la pauni
Milioni 10 itakuwa sawa tu.
Lakini Fulham yenyewe iko tayari
kukubaliana mkataba mpya na mchezaji huyo, ambaye walimchukua kutoka AZ Alkmaar
ya Uholanzi kwa daua la puni Milioni 5 mwishoni mwa msimu wa 2010.
Lakini klabu hiyo ya London, ambayo
mchezaji ghali kwao ni kipa Mark Schwarzer, inajua haiwezi kushindana na vigogo
vya England katika suala la ofa ya mshahara mnono kwa mchezaji huyo.
Dembele anachukuliwa kama moja ya
rasilimali mbili muhimu Fulham za bei mbaya, mwingine akiwa ni Clint Dempsey, ambaye
mustakabali wake klabuni hapo naye uko shakani, akiwa amebakiza mwaka mmoja
kumaliza mkataba wake.


.png)
0 comments:
Post a Comment