Published: 05th May 2012
DAVID HAYE atarejea ulingoni kutoka kwenye
kustaafu kwa kuzipiga na Dereck Chisora Julai 14, mwaka huu.
Promota Frank Warren anatarajiwa kutangaza
pambano hilo Jumanne kwenye Uwanja wa Upton Park, ambako linatarajiwa kufanyika
pambano la uzito wa Light kwa Ricky Burns kutetea ubingwa wake wa dunia dhidi
ya Kevin Mitchell.
Lakini pambano la Haye-Chisora linaweza
kuendelea japokuwa Chisora amepokonywa leseni.
Suluhisho pekee ni kwa Warren ni kufanyia
pambano hilo nje ya nchi hiyo.
Haye na Chisora bifu lao maarufu liliibuka
mjini Munich Februari katika mkutano na waandishi wa habari baada ya pambano la
Chisora na Vitali Klitschko, baada ya kuzipiga kavukavu.
Chisora ndiye aliyeanza kumzaba kibao
bingwa huyo wa WBC, hivyo akafungiwa na Bodi ya Udhibiti.
Haye aliepuka adhabu hiyo kwa sababu
alikuwa amekwishatangaza kustaafu
0 comments:
Post a Comment